ULINZI SHILIKISHI WAPUNGUZA WIZI TANDALE

Ulinzi shilikishi ulioanzishwa na viongozi wa selekeli za mitaa katika kata ya tandale umesaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa wizi wa uporaji uliokuwa umeshamili kwa kiasi kikubwa hasa nyakati za asubuhi.
Vijana hao wa ulinzi wameonekana wakifanya kazi zao vizuri na kuwakamata baadhi ya wezi wanaotaka kuiba,hivyo wa kazi wa tandale kwa sasa wako huru wanaposhuka kwenye magari na asubuhi wanapokwenda kupanda magari kwani ndio muda walio kuwa wakiporwa zaidi
Viongozi wa mitaa wanawaomba wananchi kutoa kuishilikiano kubaini waalifu na kutoa michango ya ulinzi ili zoezi hilo liwezi kudumu zaidi.

gari la polisi likimchukua mtuhumiwa aliyekamatwa na vijana wa ulinzi shilikishi tandale.

Share

WIZI TANDALE UMEKUA TISHIO

Kutokana na matukio ya wizi yanayotokea katika mitaa ya tandale imeonekana imekua tishio vitendo vya wizi,wakazi wamekua woga kutokana na vijana wengi wanaoiba kutetewa na familia zao.
ipo mitaa iliyoweka sungusungu lakini bado tatizo la wizi linatokea huku wengine wakisema wizi huu umerudi kama zamani.
jeshi la polisi linajitahidi sana kuwakamata lakini kila wakiwakamata hawakai muda wanatoka na kurudia vitendo vyao vya ualifu.

haya ni mavicho ya vibaka yaliyopo mabondeni

haya ni mavicho ya vibaka yaliyopo mabondeni

Share

WIZI ENEO LA BI MTUMWA

Katika eneo la bi mtumwa linaroanzia makaburini hadi tandale sokoni au makabiruni hadi mtogole,eneo hili ni hatali kwa wizi hasa nyakati za usiku kuanzia saa nne,pamoja na jitihada za polisi kupiga doria na kukamata lakini tatizo bado linaendelea.Wakazi wa maeneo hayo wameshafikisha malalamiko yao kwa mwenyekiti wa mtaa huo lakini hayajafanyiwa kazi..

vijana wakicheza kamali na wengine wamesimama wakiwatizama wenzao.

vijana wakicheza kamali na wengine wamesimama wakiwatizama wenzao.

tandale

Share

WIZI WARUDI TENA TANDALE

Katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu katika kata ya tandale matukio ya wizi yamejitokeza kwa wingi,katika mtaa wa muhalitani maduka matatu yamevunjwa na kuibiwa kwa nyakati tofauti na imesababisha mwenyekiti wa mtaa huo sudi makamba kuanzisha sungusungu,katika mtaa wa sokoni eneo la bimtumwa watu kila siku wanaporwa na kupigwa mapanga kitendo ambacho kinawatia hofu hasa wakazi wa eneo hiro..wizi huo sasa umekua tishio tena sana kwani vijana wanaofanya matukio hayo kutembea kwa makundi nyakati za usiku, jeshi la polisi bado halijafanikiwa kuwakamata vijana hao..

Dada huyu aliporwa

Dada huyu aliporwa

Share

WIZI BADO TATIZO KIBOKO BAR

Tatizo la wizi limekuwa tatizo katika eneo la kiboko bar,eneo hilo kuna vijana wanaokaa eneo la darajani mida ya usiku na kukaba watu,viongozi  wa mtaa wa sokoni na mtogole wameanzisha ulinzi mida ya usiku ili kuzuia tatizo hiro lakini bado haisaidii na hata wakikamatwa polisi vijana hao wanaonekana mtaani hata wiki haipiti,hivyo wanachi wamesema dawa wakipatikana kupigwa hadi kufa.IMG_0012

Share

WEZI WAKIMBIA NA PINGU

Vijana wawili wamekimbia na pingu baada ya kukamatwa..Tukio hilo limetokea mtaa wa muhalitani baada ya polisi kuwakurupusha wavuta bangi waliokuwa wamejivicha kwenye. polisi walipoingia walifanikiwa kuwakamata vijana hao wawili na kuwatia pingu, polisi wakiwa bado wanaendelea na upekuzi mle ndani ndipo vijana hao wakapata upenyo na kukimbia..Ndani ya chumba hicho vimekutwa vitu vingi vya wizi na silaha za kuibia, baada ya vijana hao kukimbia aliitwa mjumbe na kuakikisha na chumba hicho komefungwa na msako mkali ukiendelea kuwatafuta waalifu

vijana wakicheza kamali na wengine wamesimama wakiwatizama wenzao.

vijana wakicheza kamali na wengine wamesimama wakiwatizama wenzao.

Share

WIZI WATISHIA AMANI TANDALE

Wizi wa ukabaji na kutumia siraha umekua tishio katika kata ya tandale maeneo ya tanesco, kiboko bar, kwa bi mtumwa pamoja na mnarani. maeneo hayo watu wanaporwa na kukabwa na kundi linalojulikana kwa jina watoto wa road..viongozi husika wanaombwa kukomesha tabia hizo za wizi ili wananchi wawe na amani wao na mali zao pale wanapotembea njiani..

eneo hili ndio linarosifika kwa ukabaji

eneo hili ndio linarosifika kwa ukabaji

Share

WIZI TANDALE WAPUNGUA

Miongoni mwasehemu iliyokuwa ikisifika kwa wizi ni tandale, hata watu wakitajiwa jina la tandale wanaogopa , maeneo yaliyokuwa yakisifika kwa wizi ni mtogole kwa tumbo na chaka.. maeneo hayo sasa hivi yamekuwa mazuri na hakuna tena tabia hizo za wizi, haya yote yametokana na jitihada za wanachi wa tandale kwa kushilikiana na jeshi la polisi kwa kuwafichua wahalifu..

hapa wananchi wakiwa katika kikao na kujadiliana.picha na ashiru issa

hapa wananchi wakiwa katika kikao na kujadiliana.picha na ashiru issa

Share