MABOMBA YA MAJI YAMEKUWA KERO MTAANI

Mabomba ya maji ya Dawasco yamekuwa kero kutuka na kupasuka mtaani na kumwaga maji ovyo na kusababisha watu pamoja na magali kupita kwa tabu,mabomba hayo ni yale ya zamani ambayo yalikuwa hayatoi maji ila kwa sasa yameanza kutoa maji na kuzagaa mtaani.
Mabomba hayo zaidi ni eneo la Tandale Tanesco kwa bimtumwa na baadhi ya maeneo mengine tunawaona wafanya kazi wa Dawasco wakijitadi kuziba lakini baada ya muda uzibuka na kuanza kuvujisha tena.
Tunawaomba viongozi husika zoezi hili mlifanyie kazi kwani ni kero kubwa hasa tukiona maji yanazagaa huku tukiyatafuta.

hili ni shimo la maji limechimbwa kwa ajili ya kuyafunga maji yanayozagaa.

hili ni shimo la maji limechimbwa kwa ajili ya kuyafunga maji yanayozagaa.

hapa magari yakipita pembeni kupisha uzibaji wa maji

hapa magari yakipita pembeni kupisha uzibaji wa maji

mazingira

Share

OFU YATANDA JUU YA KUBOMOLEWA

Wakazi wa Tandale wanaoishi mabondeni wameingiwa na hofu juu ya kubomolewa nyumba zao, wakazi hao walishuhudia baadhi ya nyumba za bonde la mto ngombe zikiekwa alama ya kubomolewa.
Zoezi hilo la kuweka alama ndio linawatia wasiwasi wakazi wa tandale na kusikia habali zisizo lasmi kuwa ukibomolewa hakuna malipo.
Wakazi hao wamewaomba viongozi wao wa mitaa kulifuatilia zoezi hilo na waje kuwapa majibu mazuri ili wajue hatima yao..

hii ni baadhi ya nyumba iliyo mabondeni

hii ni baadhi ya nyumba iliyo mabondeni

Share

VIJANA WAJITOLEA KULINDA

Kutokana na kukidhili kwa wizi au ukubaji katika eneo la kiboko bar na bi mtumwa hadi sokoni tandale,wizi huo mala nyingi unafanyika muda wa usiku kuanzia saa 4 na kuendelea.
Watu wengi wamekabwa na kupolwa na kupigwa mapanga na makundi ya vijana hao wanaopola wanaotembea kwa makundi na silaha za jadi kuwazuru watu.
Kutokana na matukio hayo vijana wamejitolea kuweka ulinzi katika maeneo hayo nyakati za usiku,hayo yamefanyika katika kikao cha wanachi kilichofanyika eneo la tizo kilichokuwa kikijadili swala la ulinzi na usalama katika mtaa..

hapa wanachi wakiwa kwenye kikao.

hapa wanachi wakiwa kwenye kikao.

Share

BEACH BOY WALALAMIKIA KUKAMATWA

Vijana wa beach boy wa tandale bimtumwa wamelalamikia kukamatwa na polisi mara kwa mara katika kijiwa chao cha bodaboda,katika kijiwe hicho vijana hukutana na kuzungumza maswala yao mbalimbali, ndani ya mwezi huu tayari wamekamatwa mara tatu kitendo ambacho hata wateja zao wa bodaboda huogopa kuja kwa hofu ya kukamatwa..

hapa polisi wakiwa doria kwa ulinzi

hapa polisi wakiwa doria kwa ulinzi

polisi wakiwa kazini

polisi wakiwa kazini

Share

JAPO KUNA POLISI MTOGOLE FOLENI BADO TATIZO

Wakazi na wanachi wa tandale wamelalamikia tatizo la foleni linaroanzia mtogole hadi kwa tumbo, wameadai eneo hilo kuanzi asubuhi na jioni kuna polisi wa usalama barabarani lakini muda mwingi polisi hao ukamata magari badala ya kupunguza msongamano wa foleni, kwa sasa imeshakuwa mazoea asubuhi na jioni kukuta foleni maeneo hayo wanawaomba viongozi husika kulitatua la foleni maeneo hayo ambayo kwao ni kero kubwa sana..

hapa eneo la tanesco gari  zikiwa zimegongana.

hapa eneo la tanesco gari zikiwa zimegongana.

watu wakiangalia ajari ya magari yaliyogongana.

watu wakiangalia ajari ya magari yaliyogongana.

Share

MSAKO WA KUTAFUTA PANYA ROAD TANDALE

Katika kutokomeza kundi la panya road liliropata umarufu kwa muda kwa kuzuru watu na kuiba pamoja na kuua. Polisi wamefanya msako wa mfulululizo katika mitaa ya tandale na kukamata vijana wengi wa vijiweni, msako huo ulikuwa wa usiku na mchana umeleta amani na utulivu kwa wakazi wa tandale ambao waliingiwa na hofu juu ya kundi hiro na kuogopa kuzuliwa..polisi wamewaomba wananchi kutoa taalifa pale wanapoona ualifu unafanyika..

hapa polisi wakiwa doria kwa ulinzi

hapa polisi wakiwa doria kwa ulinzi

Share

SUNGUSUNGU WAUA

Sungusungu marufu kwa jina la ulinzi shilikishi, jana usiku wametumia madaraka yao vibaya na kinyume natalatibu za jeshi la polisi wamemuua deleva wa pikipiki marufu bodaboda maeneo yamanzese uzuri, walimuua kwa madai yakuwa deleva huyo alikuwa anadaiwa na mteja wake. ndipo mteja huyo alipokwenda kwenye ofisi ya sungusungu hao ili wakamkamate deleva huyo,lakini sungunsungu hao walipofika eneo la tukio hawakufuata taratibu za kisheria badala yake wakachukua sheria mkononi na kuanza kumpiga kijana huyo hadi kupoteza maisha yake.Baada ya tukio hilo wanachi wenye hasira kali walivamia ofisi ya hiyo na kualibu mali zilizipo huku wakidai wamezoea kuua leo na sisi lazima tuwaue..Ndipo polisi walipofika eneo la tukio maeneo ya manzese uzuri na kutuliza fujo hizo, pamoja na jitihada hizo wanachi walidai bado wataendelea kufanya fujo hadi kieleweke kwani sungusungu hao wamekuwa waonefu kwa wanachi..Mkuu wa upelelezi wa kituo cha ulafiki alipata nafasi na aliongea na wanachi juu ya tukio hilo, mkuu huyo aliongea mambo makuu mawili kwanza aliwaomba ladhi wanachi na kusema walichokifanya si sahihi na kinyume na taratibu za nchi na jeshi la polkisi,wote waliofanya tukio hilo watatafutwa na sheria itachukua mkondo wake..

hapa polisi na dawsco wakiwa katika msako

hapa polisi wakiwa doria kwa ulinzi

Share

DAWASCO WAKAMATA WEZI WA MAJI TANDALE

Shilika la maji nchini tanzania dawasco imekamata wezi wa maji wanaevuta maji hayo kwa kutumia pump hivo usababisha wanachi wengine kukosa maji,zoezi hilo limefanywa chini ya ulinzi mkali wa polisi kusimamia zoezi hilo, zoezi hilo limefanyika katika mitaa ya mtogole muhalitani pakacha nk.

hapa polisi na dawsco wakiwa katika msako

hapa polisi na dawsco wakiwa katika msako

 

hapa dawasco wakitoa pump kwenye nyumba ya mkazi wa mtogole

hapa dawasco wakitoa pump kwenye nyumba ya mkazi wa mtogole

 

Share