MAGARI CHAKAVU TATIZO TANDALE

Biashara ya kuuza spea za magari imekua maarufu sana hasa katika eneo la Tandale mtogole na muhalitani huku magari mabonvu yakiwa yameekwa pembeni
wakazi wa maeneo hayo wamelalamikia kitendo cha magari hayo chakavu kuwekwa pembeni inawasababishia watembea kwa miguu kupata tabu kupita huku wengine wakiwalaumu viongozi wa mtaa kulifumbia macho tatizo hiro
Wanawaomba viongozi walifanyie kazi sio kuwazuia kufanya biashara bali kutoa hayo magari chakavu pembezoni mwa barabara.

haya ni magari yaliyo kuwa pembezoni mwa barabara tandale

haya ni magari yaliyo kuwa pembezoni mwa barabara tandale

DSCF3456

Share

WIZI TANDALE UMEKUA TISHIO

Kutokana na matukio ya wizi yanayotokea katika mitaa ya tandale imeonekana imekua tishio vitendo vya wizi,wakazi wamekua woga kutokana na vijana wengi wanaoiba kutetewa na familia zao.
ipo mitaa iliyoweka sungusungu lakini bado tatizo la wizi linatokea huku wengine wakisema wizi huu umerudi kama zamani.
jeshi la polisi linajitahidi sana kuwakamata lakini kila wakiwakamata hawakai muda wanatoka na kurudia vitendo vyao vya ualifu.

haya ni mavicho ya vibaka yaliyopo mabondeni

haya ni mavicho ya vibaka yaliyopo mabondeni

Share

TANDALE NA ZOEZI LA UGAWAJI NETI

Wakazi wa tandale wameanza kuandikishwa katika zoezi la ugawaji neti au vandarua, zoezi hiro limepokelewa na changamoto nyingi huku watu wakihoji je vitakua kama vya mwanzo ngumu na vidogo huku wengine wakikataa kuandikisha na kusema kuwa vinapunguza nguvu za kiume
pamoja na changamoto zote hizo watu wamelifulahia zoezi na kusema wanasubulia kwa hamu kubwa hizo neti kwani sasa hivi neti zina bei kubwa..

hawa ni baadhi ya wandikishaji wakipokea maelezo toka kwa watendaji wa mitaa.

hawa ni baadhi ya wandikishaji wakipokea maelezo toka kwa watendaji wa mitaa.

Share

DIWANI WA TANDALE ACHAGULIWA KUWA N/MEYA K/NDONI

Diwani wa kata ya tandale mhe, Jumanne Amiri Mbunju amechaguliwa kuwa naibu meya wa manispaa ya kinondoni,uchaguzi huo uliofanyika katika jengo la manispaa na madiwani kuwachagua bwana Bonifas kuwa meya na Mbunju kuwa naibu meya.
Kwa uchaguzi huo umeweka historia ya wapinzani kuiongoza manispaa hiyo kwani haijawai kutokea toka vyama vingi vianze.

Hapa mhe, mbunju mwenye shati jeupe akiwa na mbunge wa kinondoni mhe,Mtulia..

Hapa mhe, mbunju mwenye shati jeupe akiwa na mbunge wa kinondoni mhe,Mtulia..

Share

DR MAYUYA AFARIKI DUNIA

Mwenyekiti wa ccm kata ya Tandale na kamanda wa umoja wa vijana wa ccm kata ndugu Chalres mayuya au Dr mayuya amefariki dunia nyumbani kwake tandale kwa tumbo na kuzikwa shambani kwake kibaha maili moja.
Dr mayuya alikuwa anasumbuliwa na kisukari na plesha,katika msiba wake viongozi mbalimbali wa chama walikuwepo.
Mungu ailaze loho ya malehemu mahala pema peponi amini

Hapa dr mayuya akiongozana na vijana kwenye shughuli za chama.picha na Ashiru issa

Hapa dr mayuya akiongozana na vijana kwenye shughuli za chama.picha na Ashiru issa

Share

OFU YATANDA JUU YA KUBOMOLEWA

Wakazi wa Tandale wanaoishi mabondeni wameingiwa na hofu juu ya kubomolewa nyumba zao, wakazi hao walishuhudia baadhi ya nyumba za bonde la mto ngombe zikiekwa alama ya kubomolewa.
Zoezi hilo la kuweka alama ndio linawatia wasiwasi wakazi wa tandale na kusikia habali zisizo lasmi kuwa ukibomolewa hakuna malipo.
Wakazi hao wamewaomba viongozi wao wa mitaa kulifuatilia zoezi hilo na waje kuwapa majibu mazuri ili wajue hatima yao..

hii ni baadhi ya nyumba iliyo mabondeni

hii ni baadhi ya nyumba iliyo mabondeni

Share

KIKUNDI CHA ZUIA MAFURIKO TANDALE WAJITOLEA

Wana kikundi cha zuia mafuliko Tandale wameungana na wenzao wa vikundi vya Joging kusafisha mfeleji wa kwa tumbo,zoezi hiro limefanyika siku ya sikukuu ya mauridi 24/12/2015.wakazi wa maeneo hayo wamewashukru sana kwa kujitolea kwani wameonesha moyo wa upendo.
katika zoezi hiro alialikwa mkuu wa wilaya wa Kinondoni,diwaya wa Tandale na diwani Ndugumbi.

hapa watu wakifanya kazi ya kujitolea.picha na Ashiuru issa

hapa watu wakifanya kazi ya kujitolea.picha na Ashiuru issa

Share

KARIBU X MAS NA MWAKA MPYA

Watu wengi wameonekana kwa sasa wakiwa bize kutafuta nguo za watoto kuogopa vitu kuja kupanda wakati wa sikukuu,mala nyingi sikukuu inapofika haswa hizi za dini waumini wao huwajibika kutekeleza majukumu kuakikisha na yeye anafulahi na familia yake.
Kila mtu unayemuuliza juu ya sikukuu anakwambia anaisubiri kwa hamu sana x mas kwani ni sikuku inayoambatana na mwaka mpya hivyo sina buni kuikalibisha
hayo ni maneno ya watu tuliongea nao juu ya sikukuu.
Karibu X MAS na MWAKA MPYA tunamuomba mungu atupe afya njema ili tushehelekee kwa amani na utulivu sikukuu yetu..

hapa watoto wakicheza moja ya kufulahi.pcha na Asshiru issa

hapa watoto wakicheza moja ya kufulahi.pcha na Asshiru issa

watoto wakila chakula kwenye moja ya sherehe.picha na Ashiru issa

watoto wakila chakula kwenye moja ya sherehe.picha na Ashiru issa

Share

HAPA KAZI TU

Hapa kazitu hayo ni maneno ya vijana wengi wa vijiweni kwa sasa kwani wamefulahishwa na utendaji kazi wake wa kutetea wanyonge na masikini,vijana wengi walikosa imani na serekali yao kutokana na baadhi ya vitendo vinavofanywa na baadhi ya polisi kuwakamata bila hatia.
Nao kina mama lishe wa tandale wanampongeza rais kwani lile zoezi la kukamatwa na mgambo sasa limekwisha kwani lilikuwa kero kubwa kwao lilirosababisha wengi mitaji yao kufa.
Wanamuomba rais sasa asimamie swala la ajira kwa vijana kwani ndio tatizo kubwa kwa sasa hasa kwa sisi vijana tunaomba hili alitizame kwa macho mawili jinsi ya kutusaidia sisi vijana ambao tupo wengi hatuna kazi..

hapa vijana wakiwa kijiweni wakipiga story.picha na Ashiru issa

hapa vijana wakiwa kijiweni wakipiga story.picha na Ashiru issa

Share

WAKAZI WA TANDALE WAOMBA TAKA KUZOLEWA

Wakazi wa tandale wameomba viongozi wao wafanye juu chini taka zilizokuwa barabarani zinazolewa kwa haraka,taka hizo zimewekwa barabarani baada ya jana 9/12/2015 wanachi kufanya usafi kwa kujitolea kufuatia agizo la rais.
Wanachi wamesema taka hizo zikiachwa kwa muda mlefu zinaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko na lengo la rais wetu lisifanikiwe,hivyo tunaomba mamlaka zinazohusika walifanyie kazi swala hiro.

hizi ni taka zilizowekwa barabarani.picha na Ashiru issa

hizi ni taka zilizowekwa barabarani.picha na Ashiru issa

Share