MURSHIDA NA MAENDELEO YA SOKONI

Murshida Diswele ni mwenyekiti wa mtaa wa sokoni ni mwanamke pekee aliyebahatika kuchaguliwa katika wenyeviti sita wa mitaa..Amesma katika kukabiliana na tatizo la mafuliko yeye tayali ameitisha kikao cha wananchi na kukubaliana kuchanga 2000 kila nyumba ili kutengeneza mifeleji iliyopo katika mtaa wake na tayali watu wamechanga na kufikisha laki tano na ishilini(520,000)kwa upande waliopakana na ndugumbi nako wamechanga na kufikisha laki nne (400,000) pia aliongezea ili kukabiliana na tatizo hilo wamepata mafunzo kutoka kwa mjasilia mali jinsi ya kupanda miti katika mito ili kuepuka mmongonyoko, hayo aliyasema katika hafla ya kutoa vyeti kwa vijana wa ramani huria iliyofanyika katika ofisi ya mtendaji kata tandale ..Ukweli anastahili pongezi kwa hatua hiyo aliyoifanya ikiwa viongozi waliopita walishindwa kufanya hivyo…

Share

MAFUNZO YA DAR RAMANI HURIA LEO YAMEISHA

Mafunzo waliokuwa wakipewa wanajamii wakishilikiana na wanafunzi wa chuo kikuu cha ardhi leo yamefika mwisho,mafunzo hayo yaliyodumu kwa mwezi mmoja yalikuwa kwa ajili ya kujifunza kuchora ramani pamoja na kwenda kwenye mitaa na kuhakiki picha zilizipigwa na kuchukua na taalifa nyingine muhim.katika hafla hiyo iliuzuliwa na wenyeviti wa mitaa afsa elimu pamoja na mtendaji kata na viongozi wengine walioalikwa..Wanajamii walisema ili tattizo la mafuliko liishe au kupungua tandale lazima miundo mbinu ya barabara za mitaa zijengwe ili kuweze kupitika wengine walisema makazi holela yanasababisha mafuliko,mtendaji kata aliwaomba wataalam kusaidiana kupitia elimu yao ili kumaliza hayo matatizo..

Share

KARIBU BMJ RECORD YA TANDALE

Karibu sana katika studio yetu ya bmj record iliyopo tandale kwa bimtumwa,hayo ni maneno ya muandaaji wa muziki wa kizazi kipya mr rama au rama dizo..Studio hiyo bado changa ila inakalibisha wasanii kuja kulekodi nyimbo zao, amesema haya baada ya kutembelea kwenye studio yake na kufanya mazungumzo nae, rama amesema zipo kazi mbalimbali ambazo tayari amezifanya nazinapigwa kwenye vituo vyetu vya radio..

muandaaji wa muziki rama dizo wa kwanza kushoto akiwa wenzake wakiandaa kazi.

muandaaji wa muziki rama dizo na omary wally wa mwisho ni mwandishi blog hii akiwa katika picha ya pamoja.

hapa mwandishi wa blog akijaribu kuimba na yeye

hapa mwandishi wa blog akijaribu kuimba na yeye

 

Share

DARAJA LA TANDALE, NDUGUMBI LATENGENEZWA

Dalaja linalounganisha kata ya tandale na ndugumbi lililopo mtaa wa sokoni linatalajiwa kujengwa hivi karibuni, daraja hilo ni njia kubwa inayounganisha wakazi wa ndugumbi na tandale hasa wale waenda kwa miguu. hayo yamesemwa na mjumbe wa baraza la kata na pia ni mwenyekiti selekali ya mtaa wa kwatumbo pale alipoulizwa na wanachi wa mtaa wa sokoni.

hapa ni eneo linapotaka kujengwa daraja

hapa ni eneo linapotaka kujengwa daraja

mwenyekiti wa selekali ya mtaa wa kwa tumbo

mwenyekiti wa selekali ya mtaa wa kwa tumbo

 

Share

TUNAOMBA TUWEKEWE MATUTA BARABARA YA SOKONI

Wazazi na wananchi wa mtaa wa sokoni wameomba kuwekewa matuta kwenye barabara ya tandale sokoni, barabara hiyo iliyowekwa lami hivi karibuni imekuwa tishio hasa kwa madeleva kwa kukimbiza magari bila kujari kuwa eneo hilo kuna shule, hivyo wanaomba selekali waweke matuta kwa usalama wao na watoto zao.

hapa barabara ya sokoni kabla ya kuweka lami

hapa barabara ya sokoni kabla ya kuweka lami

Share

MASHINDANO YA CHIEF CUP BADO KIPIMA JOTO

Mashindano ya mpira wa miguu ya chief cup bado ni kipima joto kwa timu zinazoshiliki.timu nyingine tayali zimejiakikishia kuingia kwenye atua ya robo fainali, huku nyingine zikingojea na kuomba dua mwenzake afungwe ili yeye apite.Ukweli mashindano hayo yamekuja na sura ya tofauti kabisa na kujizolea mashabiki wengi nyakati za jioni wakishuhudia mashindano na vipaji vya vijana chipikizi.

hapa watu wamefulika uwanjani wakitizama mpira.

hapa watu wamefulika uwanjani wakitizama mpira.

hapa napo watu wapo makini kufuatilia mchezo.

hapa napo watu wapo makini kufuatilia mchezo.

Share

KAMATI YA MASHINDANO YA CHIEF CUP YASTAHILI PONGEZI

baadhi ya wajumbe wa kamati ya mashindano ya chief cup

baadhi ya wajumbe wa kamati ya mashindano ya chief cup

Kamati ya mashindano ya chief cup yanayoendelea katika uwanja wa tandale elimu inastahili pongezi kubwa, hasa kwa kusimamia na kulatibu vizuri mashindano hayo bila kupata lawama yeyote ile.kamati hiyo ikiongozwa na YAHYA TOSTAU pamoja na VISENT BANABASI hadi sasa inafanya kazi vizuri kwa kufuata sheria na taratibu zote walizoweka.

Share