MWENYEKITI CCM WILAYA YA KINONDONI AFANYA USAFI

Mwenyekiti wa ccm wa wilaya ya kinondoni mhe, Salumu Madenge jana 4/2/2017.ameshilikiana na wakazi wa tandale katika kufanya usafi, usafi huo umefanyika katika hospital ya tandale.
zoezi hilo limefanyika huku wapenzi na wanachama wa ccm wakiwa wamevaa sale kwa ajili kuazimisha miaka 40.ya kuzaliwa ccm.
baada ya kumalizika zoezi hilo mwenyekiti aliwahutubia wanachama wate wa ccm na kutoa historia fupi ya chama kilipotoka na mazuri mengi yaliyofanywa na chama.

Huyu ni mwenyekiti wa ccm kata ya tandale mhe,Tamim omari na Ashiru issa

Share

DIWANI WA TANDALE ACHAGULIWA KUWA N/MEYA K/NDONI

Diwani wa kata ya tandale mhe, Jumanne Amiri Mbunju amechaguliwa kuwa naibu meya wa manispaa ya kinondoni,uchaguzi huo uliofanyika katika jengo la manispaa na madiwani kuwachagua bwana Bonifas kuwa meya na Mbunju kuwa naibu meya.
Kwa uchaguzi huo umeweka historia ya wapinzani kuiongoza manispaa hiyo kwani haijawai kutokea toka vyama vingi vianze.

Hapa mhe, mbunju mwenye shati jeupe akiwa na mbunge wa kinondoni mhe,Mtulia..

Hapa mhe, mbunju mwenye shati jeupe akiwa na mbunge wa kinondoni mhe,Mtulia..

Share

UCHAGUZI WAISHA KWA AMANI TANDALE

Uchaguzi uliofanyika 25/10/2015 mwaka huu katika kata ya tandale umekwisha kwa amani,uchaguzi huo ulikuwa na changamoto nyingi hasa za vijana kujitokeza kwa wingi kwenye kupiga kura, hakuna mtu aliyepigwa au kuumia zaidi ya watu kuibiwa wakiwa kwenye mikusanyiko ya watu wengi ya kushangilia ushindi wa diwani wao.hadi sasa hali ipo shwari hakuna tatizo lolote.

Hapa wananchi wakiwa kwenye mkutano wa mgombea .

Hapa wananchi wakiwa kwenye mkutano wa mgombea .

Hapa watu wakiwa kwenye foleni ya kupiga kura.

Hapa watu wakiwa kwenye foleni ya kupiga kura.

Share

KINONDONI NA MABADIRIKO

Jimbo la kinondoni limefanya mabadiriko makubwa ngazi ya kata na jimbo la kinondoni kwa ujumla,katika kata kumi za jimbo la kinondoni tayari kata sita zipo mikononi mwa upinzani na mbunge anayemaliza muda wake mhe,Iddi Azani akielekea kushindwa,mabadiriko hayo yamewafanya vijana wenge wakishangilia na kusema malofa tumeshinda..Mimi nawatakia uongozi mwema kwa wale wote waliochaguliwa katika jimbo hiro..

huyu ndie Mauridi Mtulia mgombea ubunge jimbo la kinondoni kupitia CUF

huyu ndie Mauridi Mtulia mgombea ubunge jimbo la kinondoni kupitia CUF

Share

MBUNJU KIDEDEA TANDALE

Mgombea udiwani kwa nafasi kwa tiketi ya CUF ndugu Jumanne Amiri Mbunju jana wananchi na wakazi wa tandale jana wamepiga kura na kuamua yeye ndie awe diwani wao mpya 2015-2020.katika vituo vingi vilivopigwa kura ameonekana kuongoza na kumuacha mbali mpinzani wake ndugu Tamimu O Tamimu kwa mbali..Shangwe na ndelemo zilizagaa katika mitaa yote sita ya kata ya tandale wakishangilia ushindi huo baada ya kutangazwa na msimamiza wa uchaguzi..

mwenye shati jeupe ndie MBUNJU diwani aliyeshinda tandale.

mwenye shati jeupe ndie MBUNJU diwani aliyeshinda tandale.

hawa ndio wananchi waliompa kura MBUNJU

hawa ndio wananchi waliompa kura MBUNJU

Share

VIJANA WA TANDALE NA UCHAGUZI

Vijana wengi wa kata ya tandale mwaka huu wa uchaguzi wameonekana kuhamasika na kukaa na kuzungumzia uchaguzi na wagombea wake,katika makundi mengi vijana wanamzungumzia lowasa na magufuli huku kundi kubwa la vijana likienda kumuunga mkono lowasa..sasa hivi imekuwa gumzo vijana wanapokutana na kuzungumzia siasa ni jambo ambaro miaka mitano iliyopita lilikua halina hamasa kubwa,hadi sasa hakuna taalifa yeyeyote ya vijana hao kuwa washapigana kwa ajili ya wagombea wao..mungu ibariki tanzania

k

vijana wakiwa kijiweni

Share

KAMPENI ZAANZA TANDALE

Panzia la kampeni limefunguliwa lasmi 22/08/2015 kwa vyama vote vya siasa kunadi sera zao,nafasi hiyo chama cha wanachi cuf kata ya tandale wameitumia vizuri kwa kuanza kampeni katika viwanja vya ubalozi,mnalani pamoja na kwa bimtumwa kunadi sela zao pamoja na mgombea waao,pia walisisitiza swala la amani siku ya kupiga kura..

Share

CUF TANDALE WAFULAHIA UJIO WA LOWASA

Mashabiki na wanachama wa CUF wa tandale wamefulahishwa na kitendo cha waziri mkuu mstaafu mhe,Edward lowasa kutoka ccm na kuingia ukawa,wanaamini ujio wake unaweza ukakiondoa chama cha ccm madarakani,hayo yamesemwa katika vijiwe vya wana CUF vilivyopo sokoni kwa bimtumwa,mtogole ubarozi na kwa mkunduge ilipo ngome kubwa ya CUF,vijana nao wameonekana wameamasika kwenda kujiandikisha ili kuja kupiga kura na wengine wakisema ukawa wamefanya usajili makini kumsajili lowasa..

hawa ni badhi ya vijana wakiwa kwenye foleni wakingojea kujiandikisha BVR..picha na Ashiru issa

hawa ni badhi ya vijana wakiwa kwenye foleni wakingojea kujiandikisha BVR..picha na Ashiru issa

Share