VIJANA WA MUHALITANI WAANZISHA JOGING

Vijana wapatao arobani wa mtaa wa muhalitani wamejikusanya na kuanzisha kundi la joging, lengo ni kuimalissha miili yao kwa mazoezi na hukutana pamoja kwa wiki,wanakutana mara mbili kwa wiki juma mosi na juma pili katika eneo la selekali ya mtaa wa muhalitani,kwa mara ya kwanza kikundi kama hichi kilianzishwa mtaa wa kwa tumbo na aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa huo mhe, Abdul azizi chief. Vijana hao wa muhalitani wakiwa chini ya kiongozi wao Idd Majid wanawakalibisha vijana wengine kujiunga kwani hakuna kingilio.IMG_0007

Share

HOTELI YAFUNGULIWA MUHALITANI

Hoteli imefunguliwa katika mtaa wa muhalitani inayojulikana kama jobiso fast food, hoteli hiyo imekuwa gumzo mtaani baada ya mmiliki wa hoteli hiyo kufanya tukio ambaro halitasaulika kwa kulisha watu bule siku iliyofunguliwa kuanzia asubuhi hadi hadi usiku watu walikua wakila bule..hoteli hiyo ipo muhalitani karibu na shule ya msingi tandale magharibi..IMG_0006

Share

MAKABULI YA MNARANI YAZUA UTATA

Makaburi yaliyopo mnarani mtaa wa muhalitani yamezua utata baada ya mzee na familia yake kwenda kubomoa makaburi yaliyojengewa kwa madai hawataki makaburi hayo yajengewe, hapo ndipo walipoamsha hisia za watu waliozika ndugu zao hapo na kukusanyaana na kutaka kwenda kuboa nyumba ya mzee huyo. mwenyekiti wa mtaa wa muhalitani aliongozana na polisi hadi kwa mzee huyo na kukamatwa yeye na waliohusika katika tukio hilo, huku wananchi wakipiga mayowe na wengine wakizomea na kutaka kumpiga,lakini polisi walikua imala kuzuia fujo hizo.

Share

MADAWA YA KULEVYA MIMI SASA BASI

Madawa ya kulevya mimi sasa basi, hayo ni maneno ya kijana saidi kisina anayeishi maeneo tandale muhalitani, ambaye aliyekua akitumia madawa ya kulevya zaidi ya miaka kumi, yaliyomsababishia kutengwa na familia yake pamoja na jamii na kujiingiza kwenye vitendo vya ualifu kama wizi na kunusulika kufa mala kazaa..

Ila kijana huyo kwa sasa ameamua kuacha baada ya kupata ushauri na kuamua kutumia dawa za kuzuia madawa ya kulevya, ametoa ushuhuda  huo kwa vijana wenzake ambao bado wanatumia madawa ya kulevya na kuwasihi waache waanze tiba mala moja..

huyu ndie saidi kisina aliyekua akitumia madawa ya kulevya sasa ameacha

huyu ndie saidi kisina aliyekua akitumia madawa ya kulevya sasa ameacha

Share

UFUGAJI, UZAJI WA MALI ASILI NA UTALII

Katika mtaa wa muhalitni kuna biashara ya kuleta na kusafilisha wanyama, wanyama hao wanaoletwa na kusafilishwa ni pamoja vinyonga, mijusi,nyoka,chura pamoja na ndege.wanyama hao usafilishwa kwenda nchi za nje wakiwa katika maboksi maalum.

hawa ni vinyonga wakiwa katika banda la ufugaji

hawa ni vinyonga wakiwa katika banda la ufugaji

 

haya ni maboksi wanayosafilishia wanyama hao.

haya ni maboksi wanayosafilishia wanyama hao.

 

Share

UPEPO WAZUA PAA LA NYUMBA MUHALITANI

Upepo mkari jana umezua balaa baada ya kuinua kipaa cha nyumba na kukitupia nyumba nyingine, nyumba hiyo iliyopo mtaa wa muhalitani imepatwa na balaa hilo mida ya saa 10:jioni. wananchi wa muhalitani walijitokeza kwa wingi kumsaidia muhanga huyo.pamoja na hayo hakuna aliyezulika baada ya paa hilo kuongoka.IMG_0057

hapa wanachi wakitizama nyumba iliyopatwa na maafa

hapa wanachi wakitizama nyumba iliyopatwa na maafa

Share

KIKAO CHA SHULE CHAFANYIKA

Kikao cha shule ya msingi MUHALITANI kimefanyika, kikao hicho kilichokua kikijadili utoro wa wanafunzi shuleni hapo na kuziba pengo la mwenyekiti wa shule hiyo baada ya mwenyekiti wa mwanzo kufariki dunia.wazazi kwa pamoja walimuomba mwalimu na kamati yake kuwa wakali na kutoa adhabu kali kwa wanafunzi watoro.

wanafunzi wakitoloka kwa dilishani.

wanafunzi wakitoloka kwa dilishani.

Share