MVUA IMEBOMOA NYUMBA

Mvua zilizokuwa zikinyesha imesababisha hasara kubwa kwa wakazi wa tandale maeneo ya kiboko bar na tandale kwa bi mtumwa baada ya kubomokewa na nyumba zao walizokuwa wakikaa, nyumba hizo zimebomoka mchana huku mvua zikiwa zikiendelea kunyesha,hakuna mtu yeyote yule aliyejeruhiwa na tukio hilo…IMG_0087

Share

MVUA YAZIBA BAADHI YA NJIA TANDALE

Mvua iliyonyesha kwa siku mbili mfululizo imesababisha baadhi ya njia za tandale kutopika vizuri, njia hizo ni ya chaka inayotokea mtaa wa muhalitani kuelekea sokoni tandale pamoja na dalaja la minara miwili lililopo kwa kazige mtaa wa muhalitani mpakani na mtaa wa pakacha..hali hiyo inatokea mala kwa mala hasa kipindi hichi cha mvua..IMG_3132

hapa maji yameziba njia ya wenda kwa miguu iliyozoeleka..picha na ashiru issa

hapa maji yameziba njia ya wenda kwa miguu iliyozoeleka..picha na ashiru issa

Share

TANDALE MIUNDO MBINU BADO TATIZO

Pamoja na kutengenezwa kwa mto wa ngombe na kiboko bar bado kuna tatizo la miundo mbinu hasa wakati wa mvua, usababisha mafuliko na maji kuingia hadi kwenye nyumba za watu. Hiyo imetokana na ujenzi holela bila kuzingatia utaratibu wa kuweka njia za maji na kusababisha hasara kwa watu,wakazi wa tandale wameiomba selekali kuweka utaratibu wa kuweka njia za maji ili kuondoa haza hiyo pindi mvua zinapokuja.

hapa watu wakiangalia maji yakiingia ndani ya nyumba

hapa watu wakiangalia maji yakiingia ndani ya nyumba

watu wakisindikiza uchafu uliotupwa baada ya mvua kunyesha

watu wakisindikiza uchafu uliotupwa baada ya mvua kunyesha

Share