WANAWAKE WATAKIWA KUJITAMBUA

Baadhi ya watu wametoa maoni yao juu ya siku ya wanawake na kusema wanawake wangi hawajitambui kwa hiyo wanatakiwa wapewe elimu ya utambuzi watajikinga
Katika kuchangia hoja hiyo mmoja alisema kwa mfano wangejitambua kwanza kwenye mavazi na kufanyishwa maonyesho ya kuwa uchi hii sababu kubwa hawajitambui
Pamoja na hayo yote yaliyoongeleka wamewaomba viongozi husika kuwasimamia wanawake na kuwapa elimu ya utambuzi ili kukomesha matatizo yanayojitokeza kwa wanawake.

hapa wanawake wakiwa mtaani kwenye kutunzana

hapa wanawake wakiwa mtaani kwenye kutunzana

Share

DIWANI WA TANDALE ACHAGULIWA KUWA N/MEYA K/NDONI

Diwani wa kata ya tandale mhe, Jumanne Amiri Mbunju amechaguliwa kuwa naibu meya wa manispaa ya kinondoni,uchaguzi huo uliofanyika katika jengo la manispaa na madiwani kuwachagua bwana Bonifas kuwa meya na Mbunju kuwa naibu meya.
Kwa uchaguzi huo umeweka historia ya wapinzani kuiongoza manispaa hiyo kwani haijawai kutokea toka vyama vingi vianze.

Hapa mhe, mbunju mwenye shati jeupe akiwa na mbunge wa kinondoni mhe,Mtulia..

Hapa mhe, mbunju mwenye shati jeupe akiwa na mbunge wa kinondoni mhe,Mtulia..

Share

TASAF WARUDI KWA MARA YA PILI TANDALE

Shirika la msaada la umoja wa kimataifa TASAF, Limerudi tena kwa mara ya pili tandale baada ya mala ya kwanza walikuja na kuandika kaya masikini zilizopo katika mitaa yote sita ya tandale,Hii tilip ya pili wamekuja kwa ajili ya kuhakiki watu walioandikishwa na kufanya mahojiano nao zoezi hiro limeanza jumamosi 14/03/2015 hadi juma nne 17/03/2015.zoezi hili lilikubwa na kashfa na malalamiko toka kwa wanachi na kudai wengi wao waliorozeshwa sio masikini..

picha na Ashiru issa

picha na Ashiru issa

Share

KUNA NINI KWENYE MRADI WA MAJI YETU

Mradi wa maji yetu uliokuwa ukamilike december 2013 ikashindikana ikasogezwa mbele hadi apri 2014 nayo ikashikana..Mmoja wa viongozi wa mradi huo mr Miraji alisema mradi huo umekwama kutokana na mkandalasi kushindwa kumaliza kazi zake kwa wakati, la pili mashine za maji kuchelewa kuja,mr miraji aliendelea kusema mashine hizo zishakuja na kuanzia sasa muda wowote zitafungwa.Ameyasema hayo kwenye kikao cha wana tandale club ambao walitaka kujua nini tatizo kubwa hadi mradi umekwama..

hapa mr milaji akifafanua jambo

hapa mr milaji akifafanua jambo

hapa akiwa na wana kikundi

hapa akiwa na wana kikundi

Share

AFISA ELIMU ALIA NA SEKONDARI TANDALE

Afisa elimu wa kata ya tandale ndugu Selemani mohamedi amesikitika sana baada ya kuona ndani ya kata ya tandale hakuna shule ya sekondari amewaomba wadau na mashirika yasiyo ya kiselekali kuhimizana na kulisemea kwa nguvu zote swala hili kwenye ngazi ya selekali  kwani ni jambo linalowezekana..Ameyasema alipokuwa kwenye kikao cha Tandale club kilichofanyika kwenye ukumbi wa mexico hotel..Ameaidi kushirikiana na mashirika pamoja na vikundi vya maendeleo kuona shule ya sekondari inapatikana.

wana kikundi wakiwa kwenye kikao

wana kikundi wakiwa kwenye kikao

wpid-IMG_4197.JPG

Share

UCHAGUZI MOTO TANDALE

Ikiwa imebaki miezi michache kabla ya viongozi wa selekali ya mtaa kuachia madaraka,tayari vuguvugu na joto limeanza ndani ya vyama huku chadema nao wakijipanga kuweka wagombea wao..Tandale ina mitaa sita mitaa mitano imechukuliwa na ccm na mmoja na cuf, tayari makundi ndani ya ccm yameanza kila mmoja akiwa na mgombea wake,mikutano ya hadhara ndio jukwaa pekee la kupigana vijembe huku ccm wakiwatumia viongozi wa wilaya na mkoa kujitakasa nao cuf wanamtumia diwani wa kata hiyo kujibu mapigo na kuzima moto wa ccm..Tandale ikifika wakati wa uchagizu amani huwa inapotea kwani aliyekuwa diwani wa kata hiyo dr mwilima alishawahi kupigwa wakati wa uchagizi na matukio mengi yanatokea wakati wa uchaguzi.

diwani wa kata ya tandale akieleza jambo chief akimsikiliza.

diwani wa kata ya tandale akieleza jambo chief akimsikiliza.

hapa k/mwenezi ccm kata ya tandale akihutubia

hapa k/mwenezi ccm kata ya tandale akihutubia

Share

AFISA WA AFYA AELEZA TATIZO LA TAKA TANDALE

Afisa wa afya wa Tandale ameeleza matatizo na changamoto zinazowakabili viongozi wa mitaa katika usimamiaji wa uzoaji taka,ameyasema hayo katika ukumbi wa Mexico tarehe 17/4/2014 baada ya kupokea ripoti ya mazingira kutoka katika kikundi cha Tandale club kilichopo chini ya I

hapa wana kikundi wakisikiliza maelezo toka kwa watoa mada

hapa wana kikundi wakisikiliza maelezo toka kwa watoa mada

ntergratewach.Mama afya alisema tatizo kubwa ni wakandarasi kushindwa kuendesha zoezi la uzoaji wa taka kutokana na wananchi kuwa wagumu wa kulipia ada uza taka.Mwisho aliomba ishirikiano ili kulisimamia vyema zoezi la mazingira Tandale.

Share

KARIBU KWENYE JUKWAA LA VIJANA TANDALE

Mratibu na mwandishi wa jukwaa la vijana tandale ndugu hassan pukey anawakalibisha vijana wote wa tandale katika jukwaa la vijana linalofanyika kila jumamosi, jumamosi hii jukwaa litafanyika katika ukumbi wa ofisi ya afisa mtendaji kata ya tandale muda wa saa tatu asubuhi..mgeni lasmi atakuwa diwani wa tandale ndugu jumane amiri mbunju pia watakuwepo wenyeviti wa mitaa wakisikiliza vijana wa tandale wakijadiliana.

huyu ndiye mratibu wa jukwaa la vijana hassani pukey. picha na ashiru issa

huyu ndiye mratibu wa jukwaa la vijana hassani pukey. picha na ashiru issa

Share

BARABARA YA KWA TUMBO HADI SOKONI YATIWA RAMI

Barabara inayotoka kwa tumbo kwenda hadi sokoni tandale ipo kwenye hatua za mwisho kuwekwa rami, hayo yamesemwa na mwenyekiti wa mtaa wa kwa tumbo ndugu abduly azizi (chief) kwenye mkutano..barabara hiyo iliyokuwa kero kubwa hasa kipindi cha mmvua, wafanya biashara wa soko la tandale nao wamesema imekuwa lahisi kwao kutokana na wateja wao kupata usafili tofauti na ilivokuwa mwanzo..

hapa ni eneo la sokoni kabla ya kuweka lami

hapa ni eneo la sokoni kabla ya kuweka lami.picha na ashiru issa

wanachi wakipita katika barabara ya tandale iliyowekwa mfano wa lami.picha na ashiru issa

wanachi wakipita katika barabara ya tandale iliyowekwa mfano wa lami.picha na ashiru issa

Share