BANGE ZAVUTWA HAZARANI TANDALE

katika kata ya tandale maeneo ya shule ya msingi Hekima na mtogole imekuwa kero kwa bange kuvutwa hazarani,katika eneo hilo la shule lililopo karibu na ofisi ya mtendaji wa kata bange inavutwa na kuuzwa na hazarani na kimekuwa kijiwe kikubwa cha wauzaji na wavutaji huku viongozi wakiliona hilo bila kulikemea na kusababisha wanafunzi wengine kujifunza tabia mbaya ya uvutaji wa bange, Mtogole maeneo ya stend napo bange uvutwa hazarani huku polisi wakipita na kuona bila kuchukua hatua yeyote ile,Ombi tunaomba viongozi usika maeneo hayo muyafanyie kazi ili kutokomeza tabia hiyo mbaya.

hili ndio eneo la shule linarovutwa bange

hili ndio eneo la shule linarovutwa bange

Share

MAKABULI YA MNARANI YAZUA UTATA

Makaburi yaliyopo mnarani mtaa wa muhalitani yamezua utata baada ya mzee na familia yake kwenda kubomoa makaburi yaliyojengewa kwa madai hawataki makaburi hayo yajengewe, hapo ndipo walipoamsha hisia za watu waliozika ndugu zao hapo na kukusanyaana na kutaka kwenda kuboa nyumba ya mzee huyo. mwenyekiti wa mtaa wa muhalitani aliongozana na polisi hadi kwa mzee huyo na kukamatwa yeye na waliohusika katika tukio hilo, huku wananchi wakipiga mayowe na wengine wakizomea na kutaka kumpiga,lakini polisi walikua imala kuzuia fujo hizo.

Share

Kamati ya Katiba – Tandale

Hivi karibuni kumekuwa na matangazo kutoka kwa tume ya Katiba kwa nchi nzima kupata wajumbe wa katiba kutoka katika kila kata na mitaa. Kwa Tandale kumekuwa na mwitikio mkubwa sana kwa kuwa wanatandale wengi wamejitokeza kuomba ujumbe huo wa Katiba. Zoezi hili mwisho ni Tarehe 20/03/2013 (Leo). Kama kuna mwanatanadale mwingine ambae hajaomba afanye ivo maana mwisho wa kuomba ni leo.

Share

WANA TANDALE LEO WAMETOA MAONI YAO JUU YA KATIBA MPYA

Wana tandale leo wametoa maoni yao juu ya katiba mpya. kila mmoja alitoa mchango wake na maoni yake bila kuzomewa au kuchekwa ila zaidi mtu akiongea hoja ya msingi wanampigia makofi hicho ndicho kilichofanyika tandale leo na wengine walishiliki kwa kujaza fomu na kutoa maoni  yao . hata ilipofika mwisho msimamizi alitoa sukrani za pekee kwa wana tandale kwa kutoa maoni mazuri juu ya katiba mpya na kuwasisitiza wasome vipeperushi walivyopewa kwani mchakato bado unaendelea.

Share

WANA TANDALE TUJITOKEZE KWA WINGI 26/11/2012 KUTOA MAONI YA KATIBA MPYA

Wana tandale tunatakiwa tujitokeze kwa wingi siku ya 26/11/2012 kwenye viwanja vya shule ya msingi tandale elimu ili kwenda kutoa maoni yetu juu ya katiba mpya. hii ni nafasi pekee kwetu kwani mawazo yako ni muhim sana ukipata taalifa hii mjulishe na mwenzio muda ni saa 8 mchana hadi saa 11 jioni usikose kufika.

Share