TUKO TAYARI KWA KAZI

Wahitimu wa mafunzo ya Red Croos zuia mafuliko yaliyoisha 13/11/2015 pale mexico city tandale,hayo wameyasema baada ya kuona vua zilizoanza kunyesha katika jiji la dar esalaam,wengi wao wamesema wapo tayari kuanza kufanya kazi yeyote ya zarula itayojitokeza ili kusaidia kuokoa maisha ya watu.
Wamesema mafunzo waliyopata ni muhim sana hasa kwenye jamii hivyo haipaswi kukaa nayo kimia bila kuyafanyia kazi na kuamua kuweka kauli mbiu hiyo ya tupo tayari kufanya kazi..

huyu ni miongoni mwa wanafunzi akiwaelekeza jambo wanafunzi wenzie.picha na Ashiru issa

huyu ni miongoni mwa wanafunzi akiwaelekeza jambo wanafunzi wenzie.picha na Ashiru issa

hapa mwalimu akitoa mfano wa jinsi ya kumbeba mtu aliyeumia mguu

hapa mwalimu akitoa mfano wa jinsi ya kumbeba mtu aliyeumia mguu

Share

WANA TANDALE WAPATA MAFUNZO YA HUDUMA YA KWANZA

Baadhi ya wakazi wa tandale wamepata mafunzo ya huduma ya kwanza,mafunzo yaliyofanyika katika ukumbimbi wa Mexico city uliopo tandale,mafunzo hayo yalijumuisha kata ya Tandale na Manzese yaliyoanza 9/11/2015 hadi 13/11/2015.
Miongoni mwamasomo waliojifunza nijinsi ya kumuudumia mtu aliyepata ajari,aliyeugua gafla na mtu aliyeungua na moto pamoja aliyevunjika mguu au mkono na kupata jelaha.
Mafunzo hayo yalioongozwa na walimu mahili kutoka Red Croos mhe,Mbwambo na Mauridi kapteni,katika masomo waliyotoa yaliwavutia wanafunzi na kuomba wapatapo nafasi nyingine waje kumalizia pale walipoishia.
Mafunzo hayo yamepewa jina la Red Croos Zuia mafuriko, miongoni mwa wanafunzi waliopata masomo hayo wamesema walichojifunza kwanza ni kwa faida kwao pindi watapopata matukio kama hayo watajua jinsi ya kujisaidia pili kuwasaidia watu pale wapatapo majeruhi na kuwashukuru viongozi wa Red Croos kwa kuwaletea masomo hayo ambayo ni muhimu sana kwenye jamii.

hapa wanafunzi wakijifunza jinsi ya kumbeba majeruhi.picha na Ashiru issa

hapa wanafunzi wakijifunza jinsi ya kumbeba majeruhi.picha na Ashiru issa

hii ni picha ya pamoja ya wana semina.picha na Ashiru issa

hii ni picha ya pamoja ya wana semina.picha na Ashiru issa

Share

WAZAZI WAFURAHIA UFAURU KWA WATOTO WAO

Wazazi na wakazi wa tandale wamefulahia juu ya matokeo ya ufauru wa darasa saba,imeonekana wanafunzi kufanya vizuri hasa tanzania nzima hiyo imeonekana katika maeneo ya tandale watu wakiwa bize kucheki matokeo katika simu huku wakifulahi wakiona watoto zao kufanya vizuri..

hawa ndio wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi hapa wakisikiliza jambo toka kwa walimu

hawa ndio wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi hapa wakisikiliza jambo toka kwa walimu

Share

KABANGA ATOA SOMO KWA VIJANA

Mwenyekiti wa selekali ya mtaa wa mtogole mzee kabanga ametoa somo la maisha kwa vijana,mwenyekiti ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na baadhi ya vijana wa kijiwe cha bodaboda kilichopo tanesco mwisho,Amewambia vijana hao siku zote pesa haitoshi ni vema ukaibajeti kile unachokipata ukafanyia maendeleo hivyo ndivyo tulivokuwa tunafanya sisi zamani ndio maana wazee wazamani wengi wamejenga cha pili msikae kijiweni kuilaumu selekali juu ya ajira ni vema ukajiajiri mwenyewe kama mlivofanya nyinyi kuwa madeleva wa bodaboda kuliko kungojea ajira ya selekali.Vijana nao walitoa malalamiko yao juu ya selekali kuzuia bodaboda kufika mjini kwani wateja wengi ni wamjini mwenyekiti alisema hilo ni swala la selekali kuu sisi tutalisemea kwenye vikao husika IMG_0015

Share

AFISA ELIMU ALIA NA SEKONDARI TANDALE

Afisa elimu wa kata ya tandale ndugu Selemani mohamedi amesikitika sana baada ya kuona ndani ya kata ya tandale hakuna shule ya sekondari amewaomba wadau na mashirika yasiyo ya kiselekali kuhimizana na kulisemea kwa nguvu zote swala hili kwenye ngazi ya selekali  kwani ni jambo linalowezekana..Ameyasema alipokuwa kwenye kikao cha Tandale club kilichofanyika kwenye ukumbi wa mexico hotel..Ameaidi kushirikiana na mashirika pamoja na vikundi vya maendeleo kuona shule ya sekondari inapatikana.

wana kikundi wakiwa kwenye kikao

wana kikundi wakiwa kwenye kikao

wpid-IMG_4197.JPG

Share

WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI DARASA LA NNE TANDALE WAFANYA MTIHANI

Wanafunzi wa shule za msingi tandale wamefanya mtihani wa mwaka wa kufungia shule, mitihani hiyo mala nyingi inakuwa ya kitaifa yaani tanzania nzima.wanafunzi hao wameonekana wakiwa na fulaha na mitihani inayofanyika sasa, walimu na wazazi wanawaombea wanafunzi hao wafanye vizuri ili kuepuka kufeli na kurudishwa darasa kata ya tandale ina shule nne ambazo ni tandale elimu iliyozaa shule ya msingi hekima na tandale magharibi iliyozaa shule ya msingi muhalitani.

hapa wanafunzi wakiwa nje kwa mapumziko

hapa wanafunzi wakiwa nje kwa mapumziko

Share

WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WAANZA MITIHANI

Wanafunzi wa shule za sekondari leo wameanza lasmi mitihani ya kumaliza kidato cha nne katika chi nzima, hivo wanafunzi wameombwa na wazazi pamoja na walezi kuwa makini zaidi katika kipindi hiki kigumu kwao..wanafunzi nao wameonekana kujisomea kwenye vikundi na kukumbushana baadhi ya masomo ya nyuma, tunawatakia kilala heli na masomo mema.

hapa wanafunzi wakiwasikiliza walimu pamoja na wazazi katika shelehe ya kuagwa.

hapa wanafunzi wakiwasikiliza walimu pamoja na wazazi katika shelehe ya kuagwa.

Share

WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WAAGWA

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya tuliani wamefanyiwa shelehe kuagwa ,,shelehe hiyo iliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo ziliambatana na burudani mbalimbali na wazazi nao waliwafisha mataji watoto zao..Mgeni rasmi aliwaasa wanafunzi kuwa na nidhamu ya kutosha na kuwa na bidii hasa katika kipindi hichi walicho nacho sasa,baada ya hapo mgeni alitoa vyeti kwa wanafunzi na walimu waliofanya vizuri..wanafunzi hao wanatalajiwa kufanya mtihani 4/11/2013 mwaka huu..

hapa wanafunzi wakiimba kwaya

hapa wanafunzi wakiimba kwaya

maendeleo

 

Share

KIKAO CHA SHULE CHAFANYIKA

Kikao cha shule ya msingi MUHALITANI kimefanyika, kikao hicho kilichokua kikijadili utoro wa wanafunzi shuleni hapo na kuziba pengo la mwenyekiti wa shule hiyo baada ya mwenyekiti wa mwanzo kufariki dunia.wazazi kwa pamoja walimuomba mwalimu na kamati yake kuwa wakali na kutoa adhabu kali kwa wanafunzi watoro.

wanafunzi wakitoloka kwa dilishani.

wanafunzi wakitoloka kwa dilishani.

Share