WANGE UYEE PRODUCTION BADO YATAFUTA WAZAMINI

Kundi zima la WANGE UYEE lenye masikani yake tandale muhalitani bado lipo halakati za kutafuta wadhamini ili kufanikisha malengo.kundi hiro la linalocheza michezo ya kuigiza tayari imefanikiwa kucheza michezo miwili ambayo ni ULITHI WA MOTO na NDISELA ambazo bado hawajazipatia soko la kuuza, ivyo inawaomba wadau na wapenzi wajitokeze ili kulisaidia kundi hiro ili liweze kusonga mbele..

hapa wasanii wa kundi la wange uyee wakiwa kwenye picha ya pamoja..picha na Ashiru issa

hapa wasanii wa kundi la wange uyee wakiwa kwenye picha ya pamoja..picha na Ashiru issa

Share

J,FOUR CUP YAANZA KWA MBWEMBWE

Mashindano ya mpira wa miguu yajulikanayo kama J4 CUP yameanza katika uwanja wa shule ya msingi Tandale Elimu kwa kushilikisha timu mbalimbali za tandale na nje ya tandale,kama ilivyo kawaida wakazi wa tandale ni watu wanaopenda sana michezo hasa mchezo wa soka hivyo ujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani hiyo,kwa sasa mashindano hayo yapo kwenye atua ya mzunguko..

hii ni moja ya timu shiliki

hii ni moja ya timu shiliki

hapa napo watu wapo makini kufuatilia mchezo.

hapa napo watu wapo makini kufuatilia mchezo.

Share

NI USIKU WA DAIMOND TANDALE

Baada ya kupeleka tuzo yake tandale,daimond ameamua kula idd pili na wakazi wa tandale.hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwao tandale muhalitani ulipofungwa mziki na watu kucheza.Baada ya kufika daimond aliimba baadhi ya nyimbo zake na kufanya wana tandale wamshangilie hasa pale alipoimba nyimbo ya nimpende nani watu walisema mpende wema yeye akabaki anacheka tu,aliwashukuru sana wana tandale na amesema umaarufu wake unatokana na tandale kwa hiyo awezi kuizarau tandale,ilipofika saa sita usiku hafla ilifungwa na watu walitawanyika.IMG_0012IMG_0006IMG_0013

Share

TANDALE NA BURUDANI

Kata ya tandale ni miongoni mwa kata maarufu katika wilaya ya kinondoni na inapenda sana burudani japo hakuna kumbi nyingi stalehe,mara nyingi burudani zao uzipata kama kuna harusi au watu wanatunzana au shelehe ya aina yeyote ile yenye mziki hapo ndipo utapoona watu wakimwaga lazi huku wengine wakiwa pembeni wakishangilia..burudani hizo hazichagui lika za kucheza wala hazina kualikwa wewe ukisikia mziki na umependa kucheza au kusikiliza unakalibishwa.

hapa watu wakiwa kwenye muziki wakisikiliza

hapa watu wakiwa kwenye muziki wakisikiliza

hapa watu wakicheza muziki

hapa watu wakicheza muziki

Share

(NYP)WAFANYA TAMASHA TANDALE

NETWORK OF YOUNG PEOPLE LIVING WITH HIV/AIDS(NYP)Jumamosi ya 7/9/2013 walifanya tamasha katika viwanja vya baharia vilivyopo mtaa wa pakacha maeneo ya chaka, katika tamasha hilo lilirokuwa likihusu afya ya uzazi na vijana watu wengi walijitokeza na kusikiliza, pia katika tamasha hilo kulikuwa na burudani mbalimbali kama michezo ya kuvuta kamba kukimbia na mayai maigizo pamoja na mziki, na zawadi mbalimbali zilitolewa katika tamasha hilo.

hapa mwezeshaji akitoa mada ya afya ya uzazi

hapa mwezeshaji akitoa mada ya afya ya uzazi

Share

NGOME KONGWE MBABE WA WOTE

Timu ya ngome kongwe imekua mbabe wa wote katika mashindano ya mpira wa miguu ya  chief cup. ngome kongwe imeibuka kidedea baada ya kuifunga mangoro ya tandale kwa bi mtumwa na kuwa bigwa wa mashindano hayo.fainali hiyo iliuzuliwa na viongozi wengi akiwemo diwani wa kata hiyo pamoja na viongozi wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya kinondoni.

timu ya ngome kongwe mabigwa wa chief cup

timu ya ngome kongwe mabigwa wa chief cup

diwani wa kata ya tandale akieleza jambo chief akimsikiliza.

diwani wa kata ya tandale akieleza jambo chief akimsikiliza.

abduly azizi chief akiojiwa na vyombo vya habari

abduly azizi chief akiojiwa na vyombo vya habari

Share

MASHINDANO YA CHIEF CUP BADO KIPIMA JOTO

Mashindano ya mpira wa miguu ya chief cup bado ni kipima joto kwa timu zinazoshiliki.timu nyingine tayali zimejiakikishia kuingia kwenye atua ya robo fainali, huku nyingine zikingojea na kuomba dua mwenzake afungwe ili yeye apite.Ukweli mashindano hayo yamekuja na sura ya tofauti kabisa na kujizolea mashabiki wengi nyakati za jioni wakishuhudia mashindano na vipaji vya vijana chipikizi.

hapa watu wamefulika uwanjani wakitizama mpira.

hapa watu wamefulika uwanjani wakitizama mpira.

hapa napo watu wapo makini kufuatilia mchezo.

hapa napo watu wapo makini kufuatilia mchezo.

Share

KAMATI YA MASHINDANO YA CHIEF CUP YASTAHILI PONGEZI

baadhi ya wajumbe wa kamati ya mashindano ya chief cup

baadhi ya wajumbe wa kamati ya mashindano ya chief cup

Kamati ya mashindano ya chief cup yanayoendelea katika uwanja wa tandale elimu inastahili pongezi kubwa, hasa kwa kusimamia na kulatibu vizuri mashindano hayo bila kupata lawama yeyote ile.kamati hiyo ikiongozwa na YAHYA TOSTAU pamoja na VISENT BANABASI hadi sasa inafanya kazi vizuri kwa kufuata sheria na taratibu zote walizoweka.

Share