NYANGUMI FC MABINGWA WA NGOMBE CUP

Timu ya nyangumi ya mtogole eneo la Tanesco ndio mabingwa ya mashindano yaliyoanzishwa katika uwanja wa Tandale Sokoni,ubigwa huo wameuchukua baada ya kuifunga timu ya Agentina ya manzese,Fainali hiyo iliyofanyika siku ya jumamosi 6/8/2016 uwanja wa tandale sokoni.

huyu ndie diwani wa tandale akipeana mikono na wachezaji kabla ya mechi kuanza.

huyu ndie diwani wa tandale akipeana mikono na wachezaji kabla ya mechi kuanza.


Mashindano hayo yalikuwa na kasoro nyingi hasa upande wa malefa waliokuwa wakichezesha kuonekana kupendelea, na kusababisha timu ya Sedrodi ya Tandale mnalani hawakuingiza timu kutafuta mshindi wa tatu kwa kuona wameonewa
Nyangumi inawakalibisha watu wote katika kushehelekea uubigwa wao siku ya jumamosi 13/08/2016 katika viwanja vya Tansco mwisho.
hapa mashabiki wakiwa uwanjani kabla ya mchezo kuanza

hapa mashabiki wakiwa uwanjani kabla ya mchezo kuanza

Share

S/KUU YA IDDY YAISHA KWA AMANI

watu wakila chakula kabla ya kwenda kutembea.picha na ashiru issa

watu wakila chakula kabla ya kwenda kutembea.picha na ashiru issa

e
Baada ya kufunga mwezi mtukufu na kumaliza salama tunamshukuru mungu juu ya hiro,hali hiyo imeendelea hata ilipofika sikukuu ya ya iddy wakazi wa tandale na vitongoji vyake wameshehelekea sikukuu kwa amani na utulivu tofauti na maoni ya watu walivozani.
wengi walizani kutokana na hali ya kiuchumi wizi utakuwa mwingi na ubakaji pia utakua mwingi, lakini yote hayo hayakuwepo zaidi ya watu kufulahi

Share

WIZI WARUDI TENA TANDALE

Katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu katika kata ya tandale matukio ya wizi yamejitokeza kwa wingi,katika mtaa wa muhalitani maduka matatu yamevunjwa na kuibiwa kwa nyakati tofauti na imesababisha mwenyekiti wa mtaa huo sudi makamba kuanzisha sungusungu,katika mtaa wa sokoni eneo la bimtumwa watu kila siku wanaporwa na kupigwa mapanga kitendo ambacho kinawatia hofu hasa wakazi wa eneo hiro..wizi huo sasa umekua tishio tena sana kwani vijana wanaofanya matukio hayo kutembea kwa makundi nyakati za usiku, jeshi la polisi bado halijafanikiwa kuwakamata vijana hao..

Dada huyu aliporwa

Dada huyu aliporwa

Share

USTADHI YASSNI AHIMIZA AMANI S/KUU YA IDD

Ustadhi yassini na imamu wa msikiti wa masjidi bushiri uliyopo tandale muhalitani jana wakati wa swala ya iddi amewaimiza waislamu kutenda mambo yaliyo mema na kuacha vitendo vyote viovu,sio leo umefungulia unakwenda kukesha bar unakwenda kufanya fujo na kufunja amani kwa watu wengine.Tujitahidi tuishi kwa amani kama tulivokuwa tukiishi ndani ya  mwezi mtukufu..IMG_0006

Share

WIZI WATISHIA AMANI TANDALE

Wizi wa ukabaji na kutumia siraha umekua tishio katika kata ya tandale maeneo ya tanesco, kiboko bar, kwa bi mtumwa pamoja na mnarani. maeneo hayo watu wanaporwa na kukabwa na kundi linalojulikana kwa jina watoto wa road..viongozi husika wanaombwa kukomesha tabia hizo za wizi ili wananchi wawe na amani wao na mali zao pale wanapotembea njiani..

eneo hili ndio linarosifika kwa ukabaji

eneo hili ndio linarosifika kwa ukabaji

Share

WANA TANDALE WASHELEHEKEA S/KUU YA IDD KWA AMANI

Wakazi wa tandale baada ya kuswali swala ya idd na kupata chakula cha mchana watoto kwa wakubwa wameshehelekea s/kuu ya idd kwa amani bila kutokea matatizo yoyote,mala nyingi katika s/kuu kama hizi utokea maafa ya watoto kugogwa na magari lakini hadi leo hakuna tukio lolote la ajali ya barabarani.

waumini wa kiislam wakimsikiliza shekhe akitoa hotuba ya idd

waumini wa kiislam wakimsikiliza shekhe akitoa hotuba ya idd

watoto wakitoka kupiga daku siku ya idd

watoto wakitoka kupiga daku siku ya idd

Share