MAJI YAZAGAA MTAANI TANDALE

Maji safi na salaama ya Dawasco yame kuwa kero kubwa kutokana na kuzagaa mitaani na kuababisha magari na watu kupita kwa tabu baadhi ya sehemu,tatizo hilo linakuja kutokana na mabomba kuchakaa na kuvujisha maji.
viongozi wa mitaa ujitaidi kutoa taalifa kwa watu husika na wakija wanashuhulikia tatizo na baada ya siku chache tatizo uanza tena na kuleta kero tena.
tunawaomba wanahusika kulitizama tatizo hili kwa mapama kwani maji ni muhim sana hivyo tunavyoona yanamwagika huku wengine wakiyatafuta kwa galama kubwa.
maeneo yanayomwagika maji ni muhalitani, sokoni na mtogole naamini viongozi husika watalifanyia kazi tena kwa wakati ili kuondoa usumbufu kwa wananchi.

hili ni shimo la maji limechimbwa kwa ajili ya kuyafunga maji yanayozagaa.

hili ni shimo la maji limechimbwa kwa ajili ya kuyafunga maji yanayozagaa.

Share

MTO WA NGOMBE WAFURIKA UCHAFU

Mto uliotanuliwa kwa garama kubwa ili kuepusha majanga ya mafuriko yawapatao wananchi pindi mmvua zinaponyesha.
mto huo sasa hivi umekuwa ndio dampo la watu kutupa taka japo kumepigwa marufuku kututa taka maeneo hayo.

hizi ni taka zilzotupwa kwenye bonde la mto ngombe.

hizi ni taka zilzotupwa kwenye bonde la mto ngombe.


Tunawaomba viongozi wanaohusika walitizame hili ili kuepusha adha ya magonjwa ya mlipuko na mto huo umerudidia tena kujibana endapo mmvua zitanyesha basi mafuriko huenda yakavamia nyumba za watu.

Share

MMVUA ZAANZA TAHATHALI ZITOLEWE

Msimu wa masika ndio umeanza lasmi hivyo viongozi husika wana jukumu la kuwambia wananchi wao hasa wale wanaoishi maeneo hatarishi kwa kutoa elimu na tahadhali kwa watu hao.
Mala nyingi sisi tumezoea jambo hadi litokee ndio watu wanachukua hatua wakati watu washaasilika na tukio.
Nawaomba viongozi mfanye hivyo kabla maafa hayajatokea kwa wanachi wenu .

hapa watu wakifanya kazi ya kujitoleaya kusafisha mfeleji.picha na Ashiuru issa

hapa watu wakifanya kazi ya kujitoleaya kusafisha mfeleji.picha na Ashiuru issa

Share

KUNAITAJIKA ELIMU KABLA YA MAAFA YA MAFURIKO

Tatizo la mafuriko ni janga la kitaifa mbaya zaidi halina hodi wala taalifa linapokuja, limekuwa likiwaacha watu bila makazi wengine wakipoteza maisha kutokana mafuliko
Mimi nilikuwa nawaomba viongozi wa selekali za mitaa wapewe elimu ya kuwafikishia wanachi wao au taalifa kutoka mamlaka husika juu ya majanga ya mafuriko kuliko kutegemea kusikia kwenye vyombo vya habari.

haya ni baadhi ya mafuliko watu wakitizama

haya ni baadhi ya mafuliko watu wakitizama

hapa watu wakiangalia maji yakiingia ndani ya nyumba zao na kushindwa kuyazuia

hapa watu wakiangalia maji yakiingia ndani ya nyumba zao na kushindwa kuyazuia

hapa maji yakikalibia kuingia ndani

hapa maji yakikalibia kuingia ndani

Share

TAKATAKA ZAJAA MITAANI

Zoezi la kufanya usafi kila mwezi naona limedorola hasa watu wengi kusahau hiyo siku yenyewe na kutowekea umuhim wa kujitolea kufanya usafi
Lakini pia kukosekana kwa magari ya kuzolea taka nalo imeonekana kuwa kikwazo kikubwa huku wengine wakihoji tukifanya usafi taka tunapeleka wapi
Hali isiyo ya kawaida taka zimeonekana zikiwa zimerundikana mitaani na nyingine zikiwa zinatoa wadudu, taka hizo zinatupwa vichochoroni na barabarani mida ya usiku ukitaka kujionea pita Tandale, Mwananyamala, Manzese NK.

uchafu uliotupwa pembezoni mwa ukuta..

uchafu uliotupwa pembezoni mwa ukuta..

hapa ni maeneo ya manzese taka zikiwa zimezagaa

hapa ni maeneo ya manzese taka zikiwa zimezagaa

hizi ni taka zilizotupwa barabarani.

hizi ni taka zilizotupwa barabarani.

Share

TANDALE NA ZOEZI LA UGAWAJI NETI

Wakazi wa tandale wameanza kuandikishwa katika zoezi la ugawaji neti au vandarua, zoezi hiro limepokelewa na changamoto nyingi huku watu wakihoji je vitakua kama vya mwanzo ngumu na vidogo huku wengine wakikataa kuandikisha na kusema kuwa vinapunguza nguvu za kiume
pamoja na changamoto zote hizo watu wamelifulahia zoezi na kusema wanasubulia kwa hamu kubwa hizo neti kwani sasa hivi neti zina bei kubwa..

hawa ni baadhi ya wandikishaji wakipokea maelezo toka kwa watendaji wa mitaa.

hawa ni baadhi ya wandikishaji wakipokea maelezo toka kwa watendaji wa mitaa.

Share

KIKUNDI CHA ZUIA MAFURIKO TANDALE WAJITOLEA

Wana kikundi cha zuia mafuliko Tandale wameungana na wenzao wa vikundi vya Joging kusafisha mfeleji wa kwa tumbo,zoezi hiro limefanyika siku ya sikukuu ya mauridi 24/12/2015.wakazi wa maeneo hayo wamewashukru sana kwa kujitolea kwani wameonesha moyo wa upendo.
katika zoezi hiro alialikwa mkuu wa wilaya wa Kinondoni,diwaya wa Tandale na diwani Ndugumbi.

hapa watu wakifanya kazi ya kujitolea.picha na Ashiuru issa

hapa watu wakifanya kazi ya kujitolea.picha na Ashiuru issa

Share

WAKAZI WA TANDALE WAOMBA TAKA KUZOLEWA

Wakazi wa tandale wameomba viongozi wao wafanye juu chini taka zilizokuwa barabarani zinazolewa kwa haraka,taka hizo zimewekwa barabarani baada ya jana 9/12/2015 wanachi kufanya usafi kwa kujitolea kufuatia agizo la rais.
Wanachi wamesema taka hizo zikiachwa kwa muda mlefu zinaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko na lengo la rais wetu lisifanikiwe,hivyo tunaomba mamlaka zinazohusika walifanyie kazi swala hiro.

hizi ni taka zilizowekwa barabarani.picha na Ashiru issa

hizi ni taka zilizowekwa barabarani.picha na Ashiru issa

Share

WANA TANDALE WAMUUNGA MKONO MAGUFULI

Wakazi wa tandale wameamua kujitolea na kufanya usafi katika maeneo yao ili kuweka mazingira safi na kujikinga na magonjwa yanayotokana na uchafu,hiyo imetokana na kauli iliyotolewa na mhe,Rais wa Tanzania dr magufuli aliyoisema watu wafanye usafi katika maeneo yao.
Maeneo watu waliyofanya usafi ni pamoja na mfeleji wa kiboko bar mto ngombe na mitaro yote midogo midogo ya tandale.
Wengi wao wamelizishwa na utendaji wa kazi wa rais kwa muda mchache tu toka achaguliwe,kubwa zaidi ni kuwajali masikini na wanyonge..

hii ni sehemu iliyofanyiwa usafi

hii ni sehemu iliyofanyiwa usafi

Share

TAKA ZARUNDIKANA OVYO TANDALE

Maeneo ya sokoni,mtogole pamoja na kwa tumbo,zimeonekana taka zikiwa katika marundo ya pamoja katika uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa blog hii taka hizo zimerundikana kutokana na wananchi kutangaziwa watoe taka gari linakuja,gari lilipojaa halikurudi tena na kusababisha taka hizo kubaki zimerundikana barabarani..Baadhi ya viongozi wa mitaa wanasema tatizo kubwa ni magari machache ya kuzolea taka katika mansipaa yetu ya kinondoni hiyo ni changamoto kubwa na tutaifanyia kazi ili kumaliza tatizo hili..

hizi ni taka zilizotupwa barabarani zinazosababisha ugonjwa wa kipindupindu

hizi ni taka zilizotupwa barabarani zinazosababisha ugonjwa wa kipindupindu

taka zikiwa barabarani eneo la bi mtumwa eneo la sokoni.

taka zikiwa barabarani eneo la bi mtumwa eneo la sokoni.

Share