ajali ya gari yauwa watu watatu

Ni ajali ya kutisha iliyosababisha mauaji ya watu watatu papohapo wakiwamo mtoto mmoja, mwanamke na mwanaume, gari hiyo ilikuwa inaendeshwa na kijana mwenye umri chini ya miaka 18, ambaye ni mwanafunzi wa sekondari. aliichukua gari hiyo bila ruhusa ya babu yake ambaye ni mmiliki wa gari hiyo
watu wengi walifurika kushuhudia tukio hilo ambalo si la kawaida kutokea katika maeneo haya. miongoni mwa watu waliogongwa hakuna hata mmoja aliyetambuliwa. Askari wa naohusika na uchukuaji wa maiti walichelewa sana kufika na kusababisha vurugu za hapa na pale

Pia nyumba moja iligongwa na gari hiyo na kuvunjika vibaya, bahati nzuri hakuna mtu aliyepata majeraha yoyote kwa tukio hilo

Share

2 thoughts on “ajali ya gari yauwa watu watatu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Connect with Facebook