WANA TANDALE WAPATA MAFUNZO YA HUDUMA YA KWANZA

Baadhi ya wakazi wa tandale wamepata mafunzo ya huduma ya kwanza,mafunzo yaliyofanyika katika ukumbimbi wa Mexico city uliopo tandale,mafunzo hayo yalijumuisha kata ya Tandale na Manzese yaliyoanza 9/11/2015 hadi 13/11/2015.
Miongoni mwamasomo waliojifunza nijinsi ya kumuudumia mtu aliyepata ajari,aliyeugua gafla na mtu aliyeungua na moto pamoja aliyevunjika mguu au mkono na kupata jelaha.
Mafunzo hayo yalioongozwa na walimu mahili kutoka Red Croos mhe,Mbwambo na Mauridi kapteni,katika masomo waliyotoa yaliwavutia wanafunzi na kuomba wapatapo nafasi nyingine waje kumalizia pale walipoishia.
Mafunzo hayo yamepewa jina la Red Croos Zuia mafuriko, miongoni mwa wanafunzi waliopata masomo hayo wamesema walichojifunza kwanza ni kwa faida kwao pindi watapopata matukio kama hayo watajua jinsi ya kujisaidia pili kuwasaidia watu pale wapatapo majeruhi na kuwashukuru viongozi wa Red Croos kwa kuwaletea masomo hayo ambayo ni muhimu sana kwenye jamii.

hapa wanafunzi wakijifunza jinsi ya kumbeba majeruhi.picha na Ashiru issa

hapa wanafunzi wakijifunza jinsi ya kumbeba majeruhi.picha na Ashiru issa

hii ni picha ya pamoja ya wana semina.picha na Ashiru issa

hii ni picha ya pamoja ya wana semina.picha na Ashiru issa

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Connect with Facebook