Mashindano ya kusoma Qur-an kata ya Tandale

Leo, kulikuwa na mashindano ya kusoma Qur-an ambayo yamefanyika Tandale katika mtaa wa Sokoni yakihusisha watoto wa miaka saba hadi kumi na tano. Mashindano haya mara nyingi hufanyika kipindi cha mwezi wa ramadhani, ambayo yameandaliwa na jumuiya ya vijana wa Kiislam Tandale. Hii ni kuwezesha watoto na vijana kuhifadhi maneno ya Kiislam na kuwezesha kuwa na imani ya kiislam wakiwa bado wadogo. Katika mashino hayo washindi wanategemewa kupewa zawadi kutoka kwa mgeni rasmi ambae ni Diwani wa kata ya Tandale. Mshindi wa kwanza anategemewa kupata Baiskeri, Msaafu, Juzu 3 na 35,000/-, mshindi wa pili anategemewa kupewa Baiskeri na Musahafu, na mshindi wa tatu anategemewa kupewa Pasi ya umeme, musaafu na saa ya ukutani.

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Connect with Facebook