WATOTO NA MICHEZO HATARISHI

Watoto wanahitaji uangalizi hasa katika michezo yao wanaocheza na sehemu wanazotembelea .

hapa watoto wakicheza kwenye takataka

hapa watoto wakicheza kwenye takataka


kama watoto hawa wamekutwa wakicheza katika jalala la taka ambayo ni hatari kwao kwani wanaweza kujikata au kupata magonjwa ya mlipuko nilijalibu kuwafukuza hawakutaka kunisika.
hapa watoto wakicheza kupitia dilisha la shule

hapa watoto wakicheza kupitia dilisha la shule

Share

OFU YATANDA JUU YA KUBOMOLEWA

Wakazi wa Tandale wanaoishi mabondeni wameingiwa na hofu juu ya kubomolewa nyumba zao, wakazi hao walishuhudia baadhi ya nyumba za bonde la mto ngombe zikiekwa alama ya kubomolewa.
Zoezi hilo la kuweka alama ndio linawatia wasiwasi wakazi wa tandale na kusikia habali zisizo lasmi kuwa ukibomolewa hakuna malipo.
Wakazi hao wamewaomba viongozi wao wa mitaa kulifuatilia zoezi hilo na waje kuwapa majibu mazuri ili wajue hatima yao..

hii ni baadhi ya nyumba iliyo mabondeni

hii ni baadhi ya nyumba iliyo mabondeni

Share

KIKUNDI CHA ZUIA MAFURIKO TANDALE WAJITOLEA

Wana kikundi cha zuia mafuliko Tandale wameungana na wenzao wa vikundi vya Joging kusafisha mfeleji wa kwa tumbo,zoezi hiro limefanyika siku ya sikukuu ya mauridi 24/12/2015.wakazi wa maeneo hayo wamewashukru sana kwa kujitolea kwani wameonesha moyo wa upendo.
katika zoezi hiro alialikwa mkuu wa wilaya wa Kinondoni,diwaya wa Tandale na diwani Ndugumbi.

hapa watu wakifanya kazi ya kujitolea.picha na Ashiuru issa

hapa watu wakifanya kazi ya kujitolea.picha na Ashiuru issa

Share

KARIBU X MAS NA MWAKA MPYA

Watu wengi wameonekana kwa sasa wakiwa bize kutafuta nguo za watoto kuogopa vitu kuja kupanda wakati wa sikukuu,mala nyingi sikukuu inapofika haswa hizi za dini waumini wao huwajibika kutekeleza majukumu kuakikisha na yeye anafulahi na familia yake.
Kila mtu unayemuuliza juu ya sikukuu anakwambia anaisubiri kwa hamu sana x mas kwani ni sikuku inayoambatana na mwaka mpya hivyo sina buni kuikalibisha
hayo ni maneno ya watu tuliongea nao juu ya sikukuu.
Karibu X MAS na MWAKA MPYA tunamuomba mungu atupe afya njema ili tushehelekee kwa amani na utulivu sikukuu yetu..

hapa watoto wakicheza moja ya kufulahi.pcha na Asshiru issa

hapa watoto wakicheza moja ya kufulahi.pcha na Asshiru issa

watoto wakila chakula kwenye moja ya sherehe.picha na Ashiru issa

watoto wakila chakula kwenye moja ya sherehe.picha na Ashiru issa

Share

HAPA KAZI TU

Hapa kazitu hayo ni maneno ya vijana wengi wa vijiweni kwa sasa kwani wamefulahishwa na utendaji kazi wake wa kutetea wanyonge na masikini,vijana wengi walikosa imani na serekali yao kutokana na baadhi ya vitendo vinavofanywa na baadhi ya polisi kuwakamata bila hatia.
Nao kina mama lishe wa tandale wanampongeza rais kwani lile zoezi la kukamatwa na mgambo sasa limekwisha kwani lilikuwa kero kubwa kwao lilirosababisha wengi mitaji yao kufa.
Wanamuomba rais sasa asimamie swala la ajira kwa vijana kwani ndio tatizo kubwa kwa sasa hasa kwa sisi vijana tunaomba hili alitizame kwa macho mawili jinsi ya kutusaidia sisi vijana ambao tupo wengi hatuna kazi..

hapa vijana wakiwa kijiweni wakipiga story.picha na Ashiru issa

hapa vijana wakiwa kijiweni wakipiga story.picha na Ashiru issa

Share

WAKAZI WA TANDALE WAOMBA TAKA KUZOLEWA

Wakazi wa tandale wameomba viongozi wao wafanye juu chini taka zilizokuwa barabarani zinazolewa kwa haraka,taka hizo zimewekwa barabarani baada ya jana 9/12/2015 wanachi kufanya usafi kwa kujitolea kufuatia agizo la rais.
Wanachi wamesema taka hizo zikiachwa kwa muda mlefu zinaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko na lengo la rais wetu lisifanikiwe,hivyo tunaomba mamlaka zinazohusika walifanyie kazi swala hiro.

hizi ni taka zilizowekwa barabarani.picha na Ashiru issa

hizi ni taka zilizowekwa barabarani.picha na Ashiru issa

Share

TANDALE RED CROSS NA USAFI

Kikundi cha kijamii kilichopata mafunzo ya huduma ya kwanza na kuwa wanachama wa Red cross na kujiita Tandale red cross,kikundi hicho leo kimejitolea kwenda kufanya usafi katika soko la Tandale wakishilikiana Akiba bank pamoja na wasanii mbalimbali akiwemo madii.
Shughuli hiyo iliyofanyika kuanzia saa moja asubuhi hadi saa tano asubuhi,viongongozi mbali mbali walijitokeza kujumuika na wanachi katika zoezi hilo muhimu la usafi.
Baada ya kumaliza msemaji wa Tandale red cross bwana Nasoro zee alisema lengo ni kwenda kujitolea pia na kutoa huduma ya kwanza kwa watu ambao wangeanguka,kujikata nk,lakini hadi tunamaliza zoezi hakuna aliyepata tatizo hilo.

hawa ndio wana tandale red cross.picha na  Ashiru issa

hawa ndio wana tandale red cross.picha na
Ashiru issa

Share

VIJANA WAJITOLEA KULINDA

Kutokana na kukidhili kwa wizi au ukubaji katika eneo la kiboko bar na bi mtumwa hadi sokoni tandale,wizi huo mala nyingi unafanyika muda wa usiku kuanzia saa 4 na kuendelea.
Watu wengi wamekabwa na kupolwa na kupigwa mapanga na makundi ya vijana hao wanaopola wanaotembea kwa makundi na silaha za jadi kuwazuru watu.
Kutokana na matukio hayo vijana wamejitolea kuweka ulinzi katika maeneo hayo nyakati za usiku,hayo yamefanyika katika kikao cha wanachi kilichofanyika eneo la tizo kilichokuwa kikijadili swala la ulinzi na usalama katika mtaa..

hapa wanachi wakiwa kwenye kikao.

hapa wanachi wakiwa kwenye kikao.

Share

MZEE KABANGA AMEFARIKI DUNIA

Aliyekuwa mwenyekiti wa serekali ya mtaa wa mtogole na mjumbe wa wa kamati ya siasa ccm tawi na kata, mzee Ramadhani kabanga amefariki dunia jana 5/11/2015 kwa habali tulizozipata kutoka kwa baadhi ya viongozi wanasema kifo cha Kabanga kimetokana na kudondoka alipokuwa akilima shamba huko kijijini kwake miono .
Wakazi wa tandale wengi wamepatwa na mshituko baada ya kupata taalifa ya msiba wake kabanga atakumbukwa kwa mengi hasa kwa wakazi wa mtogole kwani yeye ndie kiongozi pekee aliyepunguza kasi ya uporaji katika mtaa wa mtogole,pia alisimamia vema maswala ya maendeleo katika mtaa wake.
Mungu ailaze loho ya malehem mahala pema peponi amen.

huyu ndie mzee Kabanga mwenye kipaza sauti.mungu amlaze mahala pema peponi amini

huyu ndie mzee Kabanga mwenye kipaza sauti.mungu amlaze mahala pema peponi amini

Share

WANA TANDALE WAMUUNGA MKONO MAGUFULI

Wakazi wa tandale wameamua kujitolea na kufanya usafi katika maeneo yao ili kuweka mazingira safi na kujikinga na magonjwa yanayotokana na uchafu,hiyo imetokana na kauli iliyotolewa na mhe,Rais wa Tanzania dr magufuli aliyoisema watu wafanye usafi katika maeneo yao.
Maeneo watu waliyofanya usafi ni pamoja na mfeleji wa kiboko bar mto ngombe na mitaro yote midogo midogo ya tandale.
Wengi wao wamelizishwa na utendaji wa kazi wa rais kwa muda mchache tu toka achaguliwe,kubwa zaidi ni kuwajali masikini na wanyonge..

hii ni sehemu iliyofanyiwa usafi

hii ni sehemu iliyofanyiwa usafi

Share