TUKO TAYARI KWA KAZI

Wahitimu wa mafunzo ya Red Croos zuia mafuliko yaliyoisha 13/11/2015 pale mexico city tandale,hayo wameyasema baada ya kuona vua zilizoanza kunyesha katika jiji la dar esalaam,wengi wao wamesema wapo tayari kuanza kufanya kazi yeyote ya zarula itayojitokeza ili kusaidia kuokoa maisha ya watu.
Wamesema mafunzo waliyopata ni muhim sana hasa kwenye jamii hivyo haipaswi kukaa nayo kimia bila kuyafanyia kazi na kuamua kuweka kauli mbiu hiyo ya tupo tayari kufanya kazi..

huyu ni miongoni mwa wanafunzi akiwaelekeza jambo wanafunzi wenzie.picha na Ashiru issa

huyu ni miongoni mwa wanafunzi akiwaelekeza jambo wanafunzi wenzie.picha na Ashiru issa

hapa mwalimu akitoa mfano wa jinsi ya kumbeba mtu aliyeumia mguu

hapa mwalimu akitoa mfano wa jinsi ya kumbeba mtu aliyeumia mguu

Share

WANA TANDALE WAPATA MAFUNZO YA HUDUMA YA KWANZA

Baadhi ya wakazi wa tandale wamepata mafunzo ya huduma ya kwanza,mafunzo yaliyofanyika katika ukumbimbi wa Mexico city uliopo tandale,mafunzo hayo yalijumuisha kata ya Tandale na Manzese yaliyoanza 9/11/2015 hadi 13/11/2015.
Miongoni mwamasomo waliojifunza nijinsi ya kumuudumia mtu aliyepata ajari,aliyeugua gafla na mtu aliyeungua na moto pamoja aliyevunjika mguu au mkono na kupata jelaha.
Mafunzo hayo yalioongozwa na walimu mahili kutoka Red Croos mhe,Mbwambo na Mauridi kapteni,katika masomo waliyotoa yaliwavutia wanafunzi na kuomba wapatapo nafasi nyingine waje kumalizia pale walipoishia.
Mafunzo hayo yamepewa jina la Red Croos Zuia mafuriko, miongoni mwa wanafunzi waliopata masomo hayo wamesema walichojifunza kwanza ni kwa faida kwao pindi watapopata matukio kama hayo watajua jinsi ya kujisaidia pili kuwasaidia watu pale wapatapo majeruhi na kuwashukuru viongozi wa Red Croos kwa kuwaletea masomo hayo ambayo ni muhimu sana kwenye jamii.

hapa wanafunzi wakijifunza jinsi ya kumbeba majeruhi.picha na Ashiru issa

hapa wanafunzi wakijifunza jinsi ya kumbeba majeruhi.picha na Ashiru issa

hii ni picha ya pamoja ya wana semina.picha na Ashiru issa

hii ni picha ya pamoja ya wana semina.picha na Ashiru issa

Share

WIZI ENEO LA BI MTUMWA

Katika eneo la bi mtumwa linaroanzia makaburini hadi tandale sokoni au makabiruni hadi mtogole,eneo hili ni hatali kwa wizi hasa nyakati za usiku kuanzia saa nne,pamoja na jitihada za polisi kupiga doria na kukamata lakini tatizo bado linaendelea.Wakazi wa maeneo hayo wameshafikisha malalamiko yao kwa mwenyekiti wa mtaa huo lakini hayajafanyiwa kazi..

vijana wakicheza kamali na wengine wamesimama wakiwatizama wenzao.

vijana wakicheza kamali na wengine wamesimama wakiwatizama wenzao.

tandale

Share

TAKA ZARUNDIKANA OVYO TANDALE

Maeneo ya sokoni,mtogole pamoja na kwa tumbo,zimeonekana taka zikiwa katika marundo ya pamoja katika uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa blog hii taka hizo zimerundikana kutokana na wananchi kutangaziwa watoe taka gari linakuja,gari lilipojaa halikurudi tena na kusababisha taka hizo kubaki zimerundikana barabarani..Baadhi ya viongozi wa mitaa wanasema tatizo kubwa ni magari machache ya kuzolea taka katika mansipaa yetu ya kinondoni hiyo ni changamoto kubwa na tutaifanyia kazi ili kumaliza tatizo hili..

hizi ni taka zilizotupwa barabarani zinazosababisha ugonjwa wa kipindupindu

hizi ni taka zilizotupwa barabarani zinazosababisha ugonjwa wa kipindupindu

taka zikiwa barabarani eneo la bi mtumwa eneo la sokoni.

taka zikiwa barabarani eneo la bi mtumwa eneo la sokoni.

Share

WAZAZI WAFURAHIA UFAURU KWA WATOTO WAO

Wazazi na wakazi wa tandale wamefulahia juu ya matokeo ya ufauru wa darasa saba,imeonekana wanafunzi kufanya vizuri hasa tanzania nzima hiyo imeonekana katika maeneo ya tandale watu wakiwa bize kucheki matokeo katika simu huku wakifulahi wakiona watoto zao kufanya vizuri..

hawa ndio wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi hapa wakisikiliza jambo toka kwa walimu

hawa ndio wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi hapa wakisikiliza jambo toka kwa walimu

Share