VIJANA WA TANDALE NA UCHAGUZI

Vijana wengi wa kata ya tandale mwaka huu wa uchaguzi wameonekana kuhamasika na kukaa na kuzungumzia uchaguzi na wagombea wake,katika makundi mengi vijana wanamzungumzia lowasa na magufuli huku kundi kubwa la vijana likienda kumuunga mkono lowasa..sasa hivi imekuwa gumzo vijana wanapokutana na kuzungumzia siasa ni jambo ambaro miaka mitano iliyopita lilikua halina hamasa kubwa,hadi sasa hakuna taalifa yeyeyote ya vijana hao kuwa washapigana kwa ajili ya wagombea wao..mungu ibariki tanzania

k

vijana wakiwa kijiweni

Share

KIPINDUPINDU BADO TANDALE

Ugonjwa hatari wa kipindupindu bado haujaisha katika jiji la dare salaam hivyo imesababisha viongozi kutoa kauri za kufunga baadhi ya biashara.katika kata ya tandale nako hali si nzuri baada ya kulipotiwa kuwa na wagonjwa na kufanya migahawa ya chakula na baadhi ya maeneo kufungwa kwa muda hadi ugonjwa huo wa mlipuko utakapoisha.

hizi ni taka zilizotupwa barabarani

hizi ni taka zilizotupwa barabarani

Share

KAMPENI ZAANZA TANDALE

Panzia la kampeni limefunguliwa lasmi 22/08/2015 kwa vyama vote vya siasa kunadi sera zao,nafasi hiyo chama cha wanachi cuf kata ya tandale wameitumia vizuri kwa kuanza kampeni katika viwanja vya ubalozi,mnalani pamoja na kwa bimtumwa kunadi sela zao pamoja na mgombea waao,pia walisisitiza swala la amani siku ya kupiga kura..

Share

KIPINDUPINDU TANDALE

Wakazi wa tandale wameatazalishwa juu ya ugonjwa hatari wa kipindupindu uliozuka gafra hivi karibuni,kauli hizo zimetolewa na wenyeviti wa mitaa baada ya kupata maagizo ngazi ya wilaya na kuwatangazia wanachi wao kwa vipaza sauti na kusema kuweka usafi ili ugonjwa huo usifike,hadi leo hakuna mgonjwa yeyote yule aliyelipotiwa kufa au kuumwa ndani ya kata ya tandale..

uchafu uliotupwa pembezoni mwa ukuta..picha na ashiru issa

uchafu uliotupwa pembezoni mwa ukuta..picha na ashiru issa

Share

WIZI WARUDI TENA TANDALE

Katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu katika kata ya tandale matukio ya wizi yamejitokeza kwa wingi,katika mtaa wa muhalitani maduka matatu yamevunjwa na kuibiwa kwa nyakati tofauti na imesababisha mwenyekiti wa mtaa huo sudi makamba kuanzisha sungusungu,katika mtaa wa sokoni eneo la bimtumwa watu kila siku wanaporwa na kupigwa mapanga kitendo ambacho kinawatia hofu hasa wakazi wa eneo hiro..wizi huo sasa umekua tishio tena sana kwani vijana wanaofanya matukio hayo kutembea kwa makundi nyakati za usiku, jeshi la polisi bado halijafanikiwa kuwakamata vijana hao..

Dada huyu aliporwa

Dada huyu aliporwa

Share

CUF TANDALE WAFULAHIA UJIO WA LOWASA

Mashabiki na wanachama wa CUF wa tandale wamefulahishwa na kitendo cha waziri mkuu mstaafu mhe,Edward lowasa kutoka ccm na kuingia ukawa,wanaamini ujio wake unaweza ukakiondoa chama cha ccm madarakani,hayo yamesemwa katika vijiwe vya wana CUF vilivyopo sokoni kwa bimtumwa,mtogole ubarozi na kwa mkunduge ilipo ngome kubwa ya CUF,vijana nao wameonekana wameamasika kwenda kujiandikisha ili kuja kupiga kura na wengine wakisema ukawa wamefanya usajili makini kumsajili lowasa..

hawa ni badhi ya vijana wakiwa kwenye foleni wakingojea kujiandikisha BVR..picha na Ashiru issa

hawa ni badhi ya vijana wakiwa kwenye foleni wakingojea kujiandikisha BVR..picha na Ashiru issa

Share

MRADI WA MAJI YETU WAKAMILIKA

Mradi wa uliokua ukisuasua kwa muda mlefu na uliokuwa ukitumiwa na wana siasa wa kata ya tandale kuombea kura hatimaye sasa umekamilika, mradi wa maji yetu umekamilika baada ya vizimba vya maji kuanza kutoa huduma ya maji, huduma hiyo imeanza na changamoto nyingi huku wengine wakisusia huduma hiyo na kudai bei iliyoweka ni kubwa na wengine wakitaka kuchota bule kwa tamko la mwenyekiti wa mtaa wao, baadhi ya wanachi wamefulahishwa sana na mradi huo kukamilika kwani ilikuwa ndio kero kubwa kwao,wamewaomba viongozi wanaohusika kusimamia vizuri ili mradi huo usije ishia njiani..

hapa wakazi wa tandale wakiangalia maji yanavotoka kwenye vizimba..picha Ashiru issa

hapa wakazi wa tandale wakiangalia maji yanavotoka kwenye vizimba..picha Ashiru issa

Share

TAMIMU ANGARA TANDALE

TAMIMU OMARY TAMIMU mgombea udiwani kwenye kura za maoni ccm jana 1/08/2015.wanachama wote wa ccm walipiga kura za maoni kuchagua wabunge na madiwani,Tandale ilikuwa ni moja wapo tena ilikuwa na upinzani mkubwa kwa wale waliomba nafasi hiyo,lakini matokeo ya matawi tisa yamempa ushindi Tamimu na kumfanya angare kwa kwa kumshinda SALEHE MSHATI mtu aliyetizamiwa uenda akawa ndie mshindi..waliogombea ni
BARNABASI MKOBA
NASORO SHABANI
RAMADHANI KABANGA
ROSE MARY NYAGAWA
STALEY MASABULY
SWEDI SELEMANI
SALEHE MSHATI
TAMIMU .O. TAMIMU
ZINDUNA KIMBONEKA

Huyu ni tamimu mshindi wa kura za maoni ndani ya ccm.picha na Ashiru issa

Huyu ni tamimu mshindi wa kura za maoni ndani ya ccm.picha na Ashiru issa

Share