MURSHIDA NA MAENDELEO YA SOKONI

Murshida Diswele ni mwenyekiti wa mtaa wa sokoni ni mwanamke pekee aliyebahatika kuchaguliwa katika wenyeviti sita wa mitaa..Amesma katika kukabiliana na tatizo la mafuliko yeye tayali ameitisha kikao cha wananchi na kukubaliana kuchanga 2000 kila nyumba ili kutengeneza mifeleji iliyopo katika mtaa wake na tayali watu wamechanga na kufikisha laki tano na ishilini(520,000)kwa upande waliopakana na ndugumbi nako wamechanga na kufikisha laki nne (400,000) pia aliongezea ili kukabiliana na tatizo hilo wamepata mafunzo kutoka kwa mjasilia mali jinsi ya kupanda miti katika mito ili kuepuka mmongonyoko, hayo aliyasema katika hafla ya kutoa vyeti kwa vijana wa ramani huria iliyofanyika katika ofisi ya mtendaji kata tandale ..Ukweli anastahili pongezi kwa hatua hiyo aliyoifanya ikiwa viongozi waliopita walishindwa kufanya hivyo…

Share

WATUPA TAKA OVYO WAKAMATWA

Vijana watatu wa mtaa wa mkunduge wamekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi osterbay,vijana hao walikamatwa wakiwa na mizigo yao ya taka waliokuwa wakienda kutupa bonde la mto ngombe na kukamatwa na m/kiti wa mtaa huo na kupeleka hadi kwa watu waliowatuma kwenda kutupa nao walitiwa nguvuni na kukamatwa,hayo yalisemwa na mwenyekiti wa mtaa wa mkunduge ndugu omary kajo katika mkutano wa kufunga mafunzo ya dar ramani huria yaliyofanyika katika ofisi ya mtendaji kata ya tandale na kusisitiza ili kukomesha tatizo hiro hata muonea mtu huruma au aibu kwani tandale bila taka inawezekana,pia alisisitiza tutoe mambo ya siasa ili kuijenga tandale….

Share

MAFUNZO YA DAR RAMANI HURIA LEO YAMEISHA

Mafunzo waliokuwa wakipewa wanajamii wakishilikiana na wanafunzi wa chuo kikuu cha ardhi leo yamefika mwisho,mafunzo hayo yaliyodumu kwa mwezi mmoja yalikuwa kwa ajili ya kujifunza kuchora ramani pamoja na kwenda kwenye mitaa na kuhakiki picha zilizipigwa na kuchukua na taalifa nyingine muhim.katika hafla hiyo iliuzuliwa na wenyeviti wa mitaa afsa elimu pamoja na mtendaji kata na viongozi wengine walioalikwa..Wanajamii walisema ili tattizo la mafuliko liishe au kupungua tandale lazima miundo mbinu ya barabara za mitaa zijengwe ili kuweze kupitika wengine walisema makazi holela yanasababisha mafuliko,mtendaji kata aliwaomba wataalam kusaidiana kupitia elimu yao ili kumaliza hayo matatizo..

Share

MMVUA NA MALIPUKO YA MAGONJWA

Mmvua zinazoendelea kunyesha katika jiji zima la daresalaam zinaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko hasa kwa wakazi wa tandale,hayo yamesemwa na baadhi ya wakazi wa tandale kwa kutokana na kuwa na soko kubwa la matunda ambaro linaweza kusababisha magonjwa hayo ya mlipuko,wamewaomba viongozi wanaohusika kulifanyia kazi kabla ya kutokea maafa..

hapa ni soko la tandale kwenye matunda..picha na ashiru issa

hapa ni soko la tandale kwenye matunda..picha na ashiru issa

Share