TANDALE YA SASA SAFI

Diwani wa kata ya tandale mhe.jumanne mbunju amesema tandale ya sasa ni safi ni tandale inayopitika kila sehemu,kata hii ilikuwa na matatizo ya miundo mbinu ya barabara maji pamoja na uchafu katika mitaa,matatizo hayo kwa sasa yamepungua..Ameyasema hayo katika mkutano wa cuf uliofanyika mtaa wa mkunduge katika kuwashukuru wananchi kwa kuwachagua viongozi wa selekali ya mtaa mitatu wanaotokana na chama chao,mitaa hiyo ni kwa tumbo sokoni na mkunduge..

huyu ndie diwani wa tandale

huyu ndie diwani wa tandale

Share

KUNA NINI KWENYE MRADI WA MAJI YETU

Mradi wa maji yetu uliokuwa ukamilike december 2013 ikashindikana ikasogezwa mbele hadi apri 2014 nayo ikashikana..Mmoja wa viongozi wa mradi huo mr Miraji alisema mradi huo umekwama kutokana na mkandalasi kushindwa kumaliza kazi zake kwa wakati, la pili mashine za maji kuchelewa kuja,mr miraji aliendelea kusema mashine hizo zishakuja na kuanzia sasa muda wowote zitafungwa.Ameyasema hayo kwenye kikao cha wana tandale club ambao walitaka kujua nini tatizo kubwa hadi mradi umekwama..

hapa mr milaji akifafanua jambo

hapa mr milaji akifafanua jambo

hapa akiwa na wana kikundi

hapa akiwa na wana kikundi

Share

KURA ZATOSHA KWA MAYUYA

Uchaguzi mdogo wa ccm uliofanyika siku ya juma pili 25/1/2015 katika ofisi ya ccm kata ya tandale uchaguzi huo ulikuwa wa kuziba pengo la aliyekuwa mwenyekiti wa kata hiyo mzee muchachu aliyefaliki dunia,Wagombea wa nafasi hiyo walikuwa watatu Fatuma Mangwangwala,mr Mukele na Charles Mayuya, pamoja na mvutanno uliokuwepo kura zilitosha kumfanya charles mayuya kuwa mwenyekiti mpya wa ccm kata hiyo,shangwe na ndelemo zilishamili baada ya kutangazwa yeye mshindi,ikumbukwe kuwa mayuya hii ni mala ya pili kugombea nafasi hiyo mala ya kwanza alishindwa kwa kupata kura saba…

hapa mayuya kabla hajawa mwenyekiti wa mwisho mwenye suruali nyeupe

hapa mayuya kabla hajawa mwenyekiti wa mwisho mwenye suruali nyeupe

hapa mayuya akienda kufungua mashina ya ccm

hapa mayuya akienda kufungua mashina ya ccm

Share

PANYA ROAD WATIKISA TANDALE

Makundi ya vijana wa kihuni wanaojulikana kama panya road,mwanzoni mwa mwaka huu wamevamia maeneo ya tandale na kupola watu na vitu vyao vya samani kama simu pesa na kujeruhi watu kazaa,vijana hao wa kihuni inasemekana hawana makazi maalum walitiksa tandale takribani masaa matatu ndipo jeshi la polisi lilipo ingilia kati kwa kutumia nguvu za ziada na kupiga mabomu ya machozi ya machozi ili kuwatawanyisha wahalifu hao na kufanikiwa kuwakamata watu ishilini na tano na haikuishia hapo liliendelea siku ya pili na kukamatwa watu watano hadi sasa wapo polisi kwa kosa la uvunjifu wa amani wa watu na mali zao.

hapa polisi wakiwa doria maeneo ya chama

hapa polisi wakiwa doria maeneo ya chama

Share

UCHAGUZI WA TANDALE NA SURA MPYA

Uchaguzi uliofanyika 14/12/2014.katika kata ya tandale umeleta sura mpya,uchaguzi huo uliokuwa na fujo na vitisho na kusababisha mtaa wa kwa tumbo watu wengi kuumia na kusababisha kuzuia fujo hizo.Uchguzi huo ulioleta wenyeviti wa selekali ya mitaa wapya,mitaa yote sita na wale wa zamani kuangushwa na wengine kustafu huku chama cha CUF kikipata mitaa mitatu na CCM mitaa mitatu.

Share

ALIYETUPA MTOTO ATIWA MBARONI

Binti aliyetupa mtoto january 19..ametiwa mbaroni baada ya msako mkari wa diwani wa kata ya kijito nyama mhe:Jumanna Ulole akishilikiana na wanachi pamoja na jeshi la polisi na atimaye akatiwa nguvuni,msako huo ulikuwa nyumba kwa nyumba,chumba kwa chumba atimae akatiwa mikononi.Kwa mujibu wa msemaji mkuu wa kituo cha polisi cha Ally Maua amesema baada ya kumbana binti huyo alisema amemtupa mtoto huyo kwa shindikizo la mama yake mzazi kwa kusema hana pesa ya kumuhudumia mtoto huyo.Mpaka tunakwenda mitamboni jeshi la polisi bado linamtafuta mama mzazi wa binti huyo..IMG_1654

Share

MTOTO ATUPWA MTO WA NGOMBE

Mtu atoa mimba inayokadiliwa kuwa na miezi mitano hadi sita na kukatupa kiumbe hicho eneo la mto wa ngombe mtaa wa muhalitani,tukio hiro lilishuhudiwa na watu wengi na wengine wakisikitika kwa unyama huo uliofanywa.polisi walifika eneo la tukio na kukachukua kiumbe hicho na kuondoka nacho,katika tukio hilo yalijitokeza matukio mawili moja dada mmoja hakufahamika jina lake alikamatwa na polisi baada ya kuona hajatulia eneo la tukio wapili alizimia kwa madai yeye anatafuta mtoto wengine wanatupa watoto.IMG_3132

Share

AJALI YAUA WAWILI TANDALE TANESCO

Ajali mbaya imetokea katika eneo la tandale tanesco na kusababisha vifo vya watu wawili papo kwa papo,ajali hiyo imetokea siku ya juma pili 18/01/2015 saa mbili asubuhi imesababishwa na deleva wa boda boda kuingia mwenyewe uso kwa uso katika gari ya coster na kusababisha vifo vyao.waliyekufa wamefahamika kwa jina la Hery chande na mwingine alifahamika kwa jina moja tu dusuko dala..Eneo hili la tanesco ni hatari kwa ajari wanachi wameomba kuwekewa matuta.

moja ya ajali eneo la tanesco

moja ya ajali eneo la tanesco

Share