BANGE ZAVUTWA HAZARANI TANDALE

katika kata ya tandale maeneo ya shule ya msingi Hekima na mtogole imekuwa kero kwa bange kuvutwa hazarani,katika eneo hilo la shule lililopo karibu na ofisi ya mtendaji wa kata bange inavutwa na kuuzwa na hazarani na kimekuwa kijiwe kikubwa cha wauzaji na wavutaji huku viongozi wakiliona hilo bila kulikemea na kusababisha wanafunzi wengine kujifunza tabia mbaya ya uvutaji wa bange, Mtogole maeneo ya stend napo bange uvutwa hazarani huku polisi wakipita na kuona bila kuchukua hatua yeyote ile,Ombi tunaomba viongozi usika maeneo hayo muyafanyie kazi ili kutokomeza tabia hiyo mbaya.

hili ndio eneo la shule linarovutwa bange

hili ndio eneo la shule linarovutwa bange

Share

SUNGUSUNGU WAUA

Sungusungu marufu kwa jina la ulinzi shilikishi, jana usiku wametumia madaraka yao vibaya na kinyume natalatibu za jeshi la polisi wamemuua deleva wa pikipiki marufu bodaboda maeneo yamanzese uzuri, walimuua kwa madai yakuwa deleva huyo alikuwa anadaiwa na mteja wake. ndipo mteja huyo alipokwenda kwenye ofisi ya sungusungu hao ili wakamkamate deleva huyo,lakini sungunsungu hao walipofika eneo la tukio hawakufuata taratibu za kisheria badala yake wakachukua sheria mkononi na kuanza kumpiga kijana huyo hadi kupoteza maisha yake.Baada ya tukio hilo wanachi wenye hasira kali walivamia ofisi ya hiyo na kualibu mali zilizipo huku wakidai wamezoea kuua leo na sisi lazima tuwaue..Ndipo polisi walipofika eneo la tukio maeneo ya manzese uzuri na kutuliza fujo hizo, pamoja na jitihada hizo wanachi walidai bado wataendelea kufanya fujo hadi kieleweke kwani sungusungu hao wamekuwa waonefu kwa wanachi..Mkuu wa upelelezi wa kituo cha ulafiki alipata nafasi na aliongea na wanachi juu ya tukio hilo, mkuu huyo aliongea mambo makuu mawili kwanza aliwaomba ladhi wanachi na kusema walichokifanya si sahihi na kinyume na taratibu za nchi na jeshi la polkisi,wote waliofanya tukio hilo watatafutwa na sheria itachukua mkondo wake..

hapa polisi na dawsco wakiwa katika msako

hapa polisi wakiwa doria kwa ulinzi

Share

WAZUNGU WAFANYA ZIARA TANDALE

Mr mack na wenzie jana wamefanya ziara katika kata ya tandale mtaa wa sokoni maeneo ya chaka, katika ziara hiyo walitaka kujua jinsi athari ya mafuliko yaliyowapata wakazi wa eneo hiro..mwenyeji wao ndugu steven paul na mr msiranga waliwaeleza kwa kifupi kuwa eneo hiro ni kero kubwa wakati wa mvua usababisha watu kushindwa kupita kwenye kivuko kilichopo eneo hiro na ulazimika kuzunguka ili wafike makwao,wageni waliwapa pole wakazi wakazi wa eneo hiro na kuondoka zao..

Mark (kulia), Gary (katikati) na Ashiru (kushoto) wakitembelea maeneo ya Tandale Sokoni.

Mark (kulia), Gary (katikati) na Ashiru (kushoto) wakitembelea maeneo ya Tandale Sokoni.

Share

TAKA ZATUPWA BARABARANI KIBOKO BAR

Eneo la kiboko bar mtaa wa mtogole taka zimetupwa barabarani baada ya kusubili kwa mda mlefu gari la kutupia taka,wanachi hao walikua wakilalamikia uongozi wa mtaa kwa kushindwa zoezi la uzoaji taka japo wanawalipisha.tatizo la taka limekuwa kero kubwa hasa katika kata ya tandale ambaro bado halijapata ufumbuzi yakinifu,wakazi wengi ungojea mvua ili watupe taka au usiku kwenda kutupa barabarani kwa kivicho.

hili ndio eneo la makaburi watu wanapotupa taka

hili ndio eneo la makaburi watu wanapotupa taka

Share

ENEO LA KWA MKUNDUGE LIMEKUWA KERO

Njia inayounganisha kati ya tandale na mwananyamala eneo la mkunduge kwenda kwa manjunju limekuwa  kero kubwa kwa wakazi  eneo hiro hata wapita njia, njia hiyo imekuwa shoti kati ya magari, bajaji, bodabodaa pamoja na wenda kwa miguu. njia kwa sasa imekuwa mbovu kutokana na mvua kuaribu njia hiyo na kusababisha mashimo na maji kutwama,hivo wanachi wametoa malalamiko kwa viongozi husika ili njia hiyo ilekebishwe

hii ndio kiboko bar ya zamani.

hii ndio kiboko bar ya zamani.

Share