MKANDALASI ASHINDWA KAZI YA KUZOA TAKA

Mkandalasi aliyepewa tenda ya kuzoa taka katika mitaa ya muhalitani mtogole na mkunduge ameshindwa kulimudu zoezi hilo kutokana na kujaa kwa taka katika mitaa hiyo awali aliulizwa mkurugenzi na kudai magari yapo machache lakini watajitaidi kila wiki wapeleke gari kila mtaa, sasa yapata mwezi gari halijapita na taka zimejazana.. wanachi wanamelalamikia viongozi wao wa mtaa na kudai wanalipishwa hela za taka alafu gari haziji na kuwambia kama ameshindwa basi aseme..

hizi ni taka zilizotupwa barabarani

hizi ni taka zilizotupwa barabarani

Share

WAKAZI WA TANDALE WAJITOKEZA KWA WINGI KWENYE VITAMBULISHO VYA TAIFA

Wakazi wa tandale wamejitokeza kwa wingi kwenye vitambulisho vya taifa, zoezi hilo liliroanza 3/1/2014 na kuisha 9/1/2014 zoezi lilianza saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni..yapo matatizo yaliyojitokeza kama watu kutokuona fomu zao ikiwa majina yao yapo kwenye orodha ya majina hadi zoezi linakwisha watu hao wamepewa muongozo na kuambiwa taalifa zao zitaletwa kwa wenyeviti wa mitaa yao..

Share

HOTELI YAFUNGULIWA MUHALITANI

Hoteli imefunguliwa katika mtaa wa muhalitani inayojulikana kama jobiso fast food, hoteli hiyo imekuwa gumzo mtaani baada ya mmiliki wa hoteli hiyo kufanya tukio ambaro halitasaulika kwa kulisha watu bule siku iliyofunguliwa kuanzia asubuhi hadi hadi usiku watu walikua wakila bule..hoteli hiyo ipo muhalitani karibu na shule ya msingi tandale magharibi..IMG_0006

Share