BARABARA YA BI MTUMWA YAMWAGWA VIFUSI

Barabara ya bimtumwa inayotokea tandale sokoni kwenda hadi mtogole imewekwa vifusi na kusambaza kwa ajiri ya kuziba mashimo yaliyokuwa yamejaa katika barabara hiyo na kufanya ipitike vizuri kwa sasa..kata ya tandale ni miongoni mwa kata zitazotengenezwa  miundo mbinu ya barabara.

vifusi vikiwa vimemwagwa barabarani

vifusi vikiwa vimemwagwa barabarani

 

Share

TANDALE NA BURUDANI

Kata ya tandale ni miongoni mwa kata maarufu katika wilaya ya kinondoni na inapenda sana burudani japo hakuna kumbi nyingi stalehe,mara nyingi burudani zao uzipata kama kuna harusi au watu wanatunzana au shelehe ya aina yeyote ile yenye mziki hapo ndipo utapoona watu wakimwaga lazi huku wengine wakiwa pembeni wakishangilia..burudani hizo hazichagui lika za kucheza wala hazina kualikwa wewe ukisikia mziki na umependa kucheza au kusikiliza unakalibishwa.

hapa watu wakiwa kwenye muziki wakisikiliza

hapa watu wakiwa kwenye muziki wakisikiliza

hapa watu wakicheza muziki

hapa watu wakicheza muziki

Share

VYOO VYA SHULE YA MSINGI TANDALE ELIMU VYAZINDULIWA

Vyoo vilivokuwa vikijengwa katika shule ya msingi tandale elimu vimezinduliwa lasmi na kuanza kutumika, vyoo ivoo vilivojengwa na ufasili watu ubergiji wanaosimamia mradi wa maji yetu tandale..wafazili hao waliojenga vitu vingi tandale ikiwemo kufukua mtaro wa kiboko bar pamoja na mto ngombe. mradi huo unakalibia kwisha mwishoni mwa mwaka huu..

hapa wanafunzi wakisikiliza hotuba ya uzinduzi wa vyoo

hapa wanafunzi wakisikiliza hotuba ya uzinduzi wa vyoo

 

Share

UANDIKISHAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA WAINGIA KINONDONI

Uandikishaji wa vitambulisho vya taifa ulioanzia wilaya ya temeke ilala sasa umeingia wilaya ya kinondoni.watu na wakazi wa wilaya hiyo wanaombwa kujitokeza kwa wingi kwani zoezi hilo ni muhimu kwa kila mtanzania, kwa sasa zoezi hilo lipo katika jimbo la kawe kama wewe ni mkazi wa eneo hilo fika ofisi ya selekali ya mtaa wako utapata maelekezo yote muhimu.

haya ni majina ya watu waliondkishwa hapo awali na watu wakiakiki majina yao.

haya ni majina ya watu waliondkishwa hapo awali na watu wakiakiki majina yao.

Share

WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI DARASA LA NNE TANDALE WAFANYA MTIHANI

Wanafunzi wa shule za msingi tandale wamefanya mtihani wa mwaka wa kufungia shule, mitihani hiyo mala nyingi inakuwa ya kitaifa yaani tanzania nzima.wanafunzi hao wameonekana wakiwa na fulaha na mitihani inayofanyika sasa, walimu na wazazi wanawaombea wanafunzi hao wafanye vizuri ili kuepuka kufeli na kurudishwa darasa kata ya tandale ina shule nne ambazo ni tandale elimu iliyozaa shule ya msingi hekima na tandale magharibi iliyozaa shule ya msingi muhalitani.

hapa wanafunzi wakiwa nje kwa mapumziko

hapa wanafunzi wakiwa nje kwa mapumziko

Share

ENEO LA MKUNGUNI HATARI KWA UKABAJI

Eneo la mkunguni liliropo mtaa wa kwa pakacha njia panda ya kwenda uwanja wa fisi ni hatari sana kwa ukabaji, maeneo hayo kuna vijana upenda kukaa hapa na kuvizia watu na kuwakaba, mala nyingi uanza kukuomba hela ukiwanyima ndio wanakukaba au kukupola kama umeshika kitu..Baadhi ya wanachi wa eneo hilo wameshafikisha malalamiko yao kwa mwenyekiti wa selekari ya mtaa wa kwapakacha ili ayafanyie na kukomesha tabia hiyo..

Share

MKUTANO WA JUMUIYA YA WAZAZI KWA TUMBO WAFANA

Mkutano wa jumuiya ya wazazi kwa tumbo uliofanyika jana 10/11/2013 umefana na umekua wa aina yake, mkutano huo uliokua umepambwa na burudani mbalimbali na kuudhuliwa na viongozi wa kata na wilaya, mgeni rasmi katika mkutano huo alikua mwenyekiti wa wazazi wilaya ya kinondoni ndugu charles mgonja aliyetoa taalifa ya utekelezaji wa chama katika kata ya tandale..

huyu mwenyekiti wa wazazi wilaya ya kinondoni

huyu mwenyekiti wa wazazi wilaya ya kinondoni

hapa viongozi wakifuatilia mkutano kwa kalibu

hapa viongozi wakifuatilia mkutano kwa kalibu

Share

JUMUIYA YA WAZAZI KWA TUMBO LEO YAFANYA MKUTANO WA HADHARA

Jumuiya ya wazazi ya ccm ya kwa tumbo leo wanafanya mkutano wa hadhara, mkutano huo utafanyika katika viwanja vya ccm kwa tumbo kuanzia saa 8:30 mchana.viongozi wa chama ngazi ya kata na wilaya watakuwepo katika mkatano huo, lengo la mkutano huo ni kushukuru wanachama  wa jumuiya na kueleza mafanikio yaliyofanywa na chama katika mtaa huo..

huyu ni mwenyekiti wa s/mtaa kwa tumbo akieleza jambo kwa wana ccm huku m/kiti ccm wilaya nae akmsikiliza.

huyu ni mwenyekiti wa s/mtaa kwa tumbo akieleza jambo kwa wana ccm huku m/kiti ccm wilaya nae akmsikiliza.

Share

WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WAANZA MITIHANI

Wanafunzi wa shule za sekondari leo wameanza lasmi mitihani ya kumaliza kidato cha nne katika chi nzima, hivo wanafunzi wameombwa na wazazi pamoja na walezi kuwa makini zaidi katika kipindi hiki kigumu kwao..wanafunzi nao wameonekana kujisomea kwenye vikundi na kukumbushana baadhi ya masomo ya nyuma, tunawatakia kilala heli na masomo mema.

hapa wanafunzi wakiwasikiliza walimu pamoja na wazazi katika shelehe ya kuagwa.

hapa wanafunzi wakiwasikiliza walimu pamoja na wazazi katika shelehe ya kuagwa.

Share