MKUTANO WA MAJI YETU WAFANYIKA TANDALE

Mradi wa maji yetu tandale ukikalibia kumalizika na kukabiziwa kwa wanachi wenyewe, viongozi na wanachama wa mradi huo wamefanya mkutano 26/10/2013 katika shule ya msingi elimu..mkutano huo ulikuwa wa kujadili maagizo ya wafaziri wanaotaka kuwe na viongozi wa kuajiliwa na viongozi wa vizimba wao kazi yao itakuwa ni kusimamia mradi huo..Hoja hiyo ilizua mjadala mkubwa huku watu wengine wakipinga utalatibu wa kuwa na viongozi wa kuajiliwa, baada ya mvutano mkubwa wote kwa pamoja walikubaliana kuwepo kwa utaratibu huo.

hapa wanachaama wakiwa kwenye mkutano

hapa wanachaama wakiwa kwenye mkutano

Share

MIUNDO MBINU YAJA TANDALE

hii ni alama ya kubomoa

hii ni alama ya kubomoa

Nyumba nyingi zilizopo tandale zimewekwa alama ya kubomolewa ili kupisha ujenzi wa barabara za mitaa..kila mwenye nyumba aliyeasilika na zoezi hiro amepewa kalatasi ya kujaza na akimaliza aipeleke kwenye ofisi ya mtendaji kata, wengi wamefulahia zoezi hilo ila wasiwasi wao upo kwenye malipo watakayopewa..IMG_0097

Share

WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WAAGWA

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya tuliani wamefanyiwa shelehe kuagwa ,,shelehe hiyo iliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo ziliambatana na burudani mbalimbali na wazazi nao waliwafisha mataji watoto zao..Mgeni rasmi aliwaasa wanafunzi kuwa na nidhamu ya kutosha na kuwa na bidii hasa katika kipindi hichi walicho nacho sasa,baada ya hapo mgeni alitoa vyeti kwa wanafunzi na walimu waliofanya vizuri..wanafunzi hao wanatalajiwa kufanya mtihani 4/11/2013 mwaka huu..

hapa wanafunzi wakiimba kwaya

hapa wanafunzi wakiimba kwaya

maendeleo

 

Share

U.W.T TANDALE WAFANYA MKUTANO

Umoja wa wanawake tanzania U.W.T 27/10/2013 walifanya mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa ccm mashuka..Mkutano huo uliohudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwepo mwenyekiti wa ccm wilaya ya kinondoni ndugu. SALUM MADENGE watu walifulika katika mkutano huo na wenyeviti wa selekali za mitaa wanaotokana na ccm nao walipata fulsa ya kuzungumza na kusema maendeleo yaliyofanywa na chama, na kueleza uboleshaji wa miundo mbinu ya barabara inayofanyika na itayofanyika tandale.

hapa k/mwenezi ccm kata ya tandale akihutubia

hapa k/mwenezi ccm kata ya tandale akihutubia

Share

MAKABULI YA MNARANI YAZUA UTATA

Makaburi yaliyopo mnarani mtaa wa muhalitani yamezua utata baada ya mzee na familia yake kwenda kubomoa makaburi yaliyojengewa kwa madai hawataki makaburi hayo yajengewe, hapo ndipo walipoamsha hisia za watu waliozika ndugu zao hapo na kukusanyaana na kutaka kwenda kuboa nyumba ya mzee huyo. mwenyekiti wa mtaa wa muhalitani aliongozana na polisi hadi kwa mzee huyo na kukamatwa yeye na waliohusika katika tukio hilo, huku wananchi wakipiga mayowe na wengine wakizomea na kutaka kumpiga,lakini polisi walikua imala kuzuia fujo hizo.

Share

TANDALE MIUNDO MBINU BADO TATIZO

Pamoja na kutengenezwa kwa mto wa ngombe na kiboko bar bado kuna tatizo la miundo mbinu hasa wakati wa mvua, usababisha mafuliko na maji kuingia hadi kwenye nyumba za watu. Hiyo imetokana na ujenzi holela bila kuzingatia utaratibu wa kuweka njia za maji na kusababisha hasara kwa watu,wakazi wa tandale wameiomba selekali kuweka utaratibu wa kuweka njia za maji ili kuondoa haza hiyo pindi mvua zinapokuja.

hapa watu wakiangalia maji yakiingia ndani ya nyumba

hapa watu wakiangalia maji yakiingia ndani ya nyumba

watu wakisindikiza uchafu uliotupwa baada ya mvua kunyesha

watu wakisindikiza uchafu uliotupwa baada ya mvua kunyesha

Share