INTERGRITY WATCH WAFANYA KIKAO

Shilika lisilo la kiselekali la intergrity watch jana wamefanya kikao na wanakikundi cha tandale na kuwajulisha kuwa 17/10/2013 kutakuwa na ugeni utaotoka katika ofisi zao kuja kwatembelea na kutazama maendeleo ya kikundi..Wana kikundi nao walilipokea kwa fulaha jambo hilo na kuamasishana kuwahi siku ya tukio.

hapa wana kikundi wakiwa katika picha ya pamoja

hapa wana kikundi wakiwa katika picha ya pamoja

hapa wana kikundi wakisikiliza maelezo toka kwa watoa mada

hapa wana kikundi wakisikiliza maelezo toka kwa watoa mada

Share

KARIBU BMJ RECORD YA TANDALE

Karibu sana katika studio yetu ya bmj record iliyopo tandale kwa bimtumwa,hayo ni maneno ya muandaaji wa muziki wa kizazi kipya mr rama au rama dizo..Studio hiyo bado changa ila inakalibisha wasanii kuja kulekodi nyimbo zao, amesema haya baada ya kutembelea kwenye studio yake na kufanya mazungumzo nae, rama amesema zipo kazi mbalimbali ambazo tayari amezifanya nazinapigwa kwenye vituo vyetu vya radio..

muandaaji wa muziki rama dizo wa kwanza kushoto akiwa wenzake wakiandaa kazi.

muandaaji wa muziki rama dizo na omary wally wa mwisho ni mwandishi blog hii akiwa katika picha ya pamoja.

hapa mwandishi wa blog akijaribu kuimba na yeye

hapa mwandishi wa blog akijaribu kuimba na yeye

 

Share

MADAWA YA KULEVYA MIMI SASA BASI

Madawa ya kulevya mimi sasa basi, hayo ni maneno ya kijana saidi kisina anayeishi maeneo tandale muhalitani, ambaye aliyekua akitumia madawa ya kulevya zaidi ya miaka kumi, yaliyomsababishia kutengwa na familia yake pamoja na jamii na kujiingiza kwenye vitendo vya ualifu kama wizi na kunusulika kufa mala kazaa..

Ila kijana huyo kwa sasa ameamua kuacha baada ya kupata ushauri na kuamua kutumia dawa za kuzuia madawa ya kulevya, ametoa ushuhuda  huo kwa vijana wenzake ambao bado wanatumia madawa ya kulevya na kuwasihi waache waanze tiba mala moja..

huyu ndie saidi kisina aliyekua akitumia madawa ya kulevya sasa ameacha

huyu ndie saidi kisina aliyekua akitumia madawa ya kulevya sasa ameacha

Share

(NYP)WAFANYA TAMASHA TANDALE

NETWORK OF YOUNG PEOPLE LIVING WITH HIV/AIDS(NYP)Jumamosi ya 7/9/2013 walifanya tamasha katika viwanja vya baharia vilivyopo mtaa wa pakacha maeneo ya chaka, katika tamasha hilo lilirokuwa likihusu afya ya uzazi na vijana watu wengi walijitokeza na kusikiliza, pia katika tamasha hilo kulikuwa na burudani mbalimbali kama michezo ya kuvuta kamba kukimbia na mayai maigizo pamoja na mziki, na zawadi mbalimbali zilitolewa katika tamasha hilo.

hapa mwezeshaji akitoa mada ya afya ya uzazi

hapa mwezeshaji akitoa mada ya afya ya uzazi

Share

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MRADI TANDALE

Mwenge wa uhuru jana 4/9/2013 umezindua mradi wa maji yetu uliopo tandale, mradi huo utakao gawa maji kata nzima ya tandale unatalajiwa kukamilika mwezi wa kumi mwaka huu, katika uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi tandale muhalitani watu walijitokeza kwa wingi kuja kuuona mwenge na kusikiliza maneno ya viongozi.

huu ndio mwenge wa uhuru uliozindua mradi

huu ndio mwenge wa uhuru uliozindua mradi

kiongozi wa mbio za mwenge akibadilishana mawzo na mkuu wa wilaya ya kinondoni huku diwani wa tandale akiwa nyuma yao

kiongozi wa mbio za mwenge akibadilishana mawzo na mkuu wa wilaya ya kinondoni huku diwani wa tandale akiwa nyuma yao

wanafunzi wakimsikiliza kiongozi wa mbio za mwenge.

wanafunzi wakimsikiliza kiongozi wa mbio za mwenge.

Share