UPEPO WAZUA PAA LA NYUMBA MUHALITANI

Upepo mkari jana umezua balaa baada ya kuinua kipaa cha nyumba na kukitupia nyumba nyingine, nyumba hiyo iliyopo mtaa wa muhalitani imepatwa na balaa hilo mida ya saa 10:jioni. wananchi wa muhalitani walijitokeza kwa wingi kumsaidia muhanga huyo.pamoja na hayo hakuna aliyezulika baada ya paa hilo kuongoka.IMG_0057

hapa wanachi wakitizama nyumba iliyopatwa na maafa

hapa wanachi wakitizama nyumba iliyopatwa na maafa

Share

DARAJA LA TANDALE, NDUGUMBI LATENGENEZWA

Dalaja linalounganisha kata ya tandale na ndugumbi lililopo mtaa wa sokoni linatalajiwa kujengwa hivi karibuni, daraja hilo ni njia kubwa inayounganisha wakazi wa ndugumbi na tandale hasa wale waenda kwa miguu. hayo yamesemwa na mjumbe wa baraza la kata na pia ni mwenyekiti selekali ya mtaa wa kwatumbo pale alipoulizwa na wanachi wa mtaa wa sokoni.

hapa ni eneo linapotaka kujengwa daraja

hapa ni eneo linapotaka kujengwa daraja

mwenyekiti wa selekali ya mtaa wa kwa tumbo

mwenyekiti wa selekali ya mtaa wa kwa tumbo

 

Share

TUNAOMBA TUWEKEWE MATUTA BARABARA YA SOKONI

Wazazi na wananchi wa mtaa wa sokoni wameomba kuwekewa matuta kwenye barabara ya tandale sokoni, barabara hiyo iliyowekwa lami hivi karibuni imekuwa tishio hasa kwa madeleva kwa kukimbiza magari bila kujari kuwa eneo hilo kuna shule, hivyo wanaomba selekali waweke matuta kwa usalama wao na watoto zao.

hapa barabara ya sokoni kabla ya kuweka lami

hapa barabara ya sokoni kabla ya kuweka lami

Share

TAKA ZATUPWA BARABARANI KIBOKO BAR

pamoja na juhudi za selekali kutengeneza barabara ya kiboko bar iliyokuwa kero kubwa kwa wakazi wa tandale sasa barabara hiyo imekwisha na inapitika, lakini imekuwa dampo kwa watu kutupa taka barabarani na kufanya taka zizagae ovyo wakati ni atali kwa afya.mwenyekiti wa mtaa wa mtogole na muhalitani tayali wameeka ulinzi na azabu kali kwa atayekamatwa akitupa taka katika maeneo hayo.

hizi ni taka zilizotupwa barabarani kiboko bar

hizi ni taka zilizotupwa barabarani kiboko bar

 

Share

VIJANA WANZISHA ULINZI SHILIKISHI KUKOMESHA WIZI

Vijana wa mtogole wameanzisha vikosi vya ulinzi shilikishi ili kukomesha wizi unaotokea mara kwa mara nyakati za usiku. katika mwezi huu yametokea matukio ya wizi na kusababisha watu kuporwa na magari kutekwa usiku na kuvamia na kuibiwa na matukio hayo yote yamefanyika tandale. vijana hao wameamua kufanya hivyo kwa kujitolea  na wameungwa mkono na viongozi wa selekali pamoja na wanachi wa tandale.

hapa polisi wakiwa doria maeneo ya chama

hapa polisi wakiwa doria maeneo ya chama

hapa wanachi wakishuhudia mwizi akichukuliwa na polisi.

hapa wanachi wakishuhudia mwizi akichukuliwa na polisi.

Share

ENEO LA CHAMA YEMENI NA TANESCO YANAONGOZA KWA AJARI TANDALE

Maeneo ya chama yemeni ya mtaa wa mkunduge pamoja na tanesco ya mtaa wa mtogole yanaongoza kwa ajali za barabarani.maeneo hayo utokea ajari mara kwa mara na usababisha watu kufa na wengine kupata vilema, tunaomba viongozi husika sehemu hizo wafanye utaratibu wa kuweka matuta.

hapa eneo la tanesco gari  zikiwa zimegongana.

hapa eneo la tanesco gari zikiwa zimegongana.

hapa askari akipima ajari ya barabarani

hapa askari akipima ajari ya barabarani

Share

SOKO LA TANDALE LAKALABATIWA

Njia ya inayokwenda sokoni tandale kupitia kwa tumbo imekalabatiwa kwa kuweka vifusi na eneo la soko ikiwekwa lami chafu, barabara hiyo iliyokua imealibika sana kipindi cha mvua na kushindwa kupitika na kufanya eneo la soko kuwa chafu, hivi sasa inapitika ila ingewekwa matuta kwa usalama zaidi kwa waenda kwa miguu.

hapa ni eneo la sosko la tandale palipowekwa lami chafu.

hapa ni eneo la sosko la tandale palipowekwa lami chafu.

wanachi wakipita katika barabara ya tandale iliyotengenezwa.

wanachi wakipita katika barabara ya tandale iliyotengenezwa.

Share

BARABARA YA TANDALE UZURI YAZIBWA VIRAKA

Barabara ya tandale uzuri imetengenezwa kwa kulepewa kwa zile sehemu zilizochimbika na kuweka lami mpya, barabara hiyo ilikua imealibika kutokana na mvua zilizokua zikinyesha na kufanya iwe na mashimo kile sehemu, wakazi wa tandale wameishukuru selekali kwa ukalabati huo.

hapa barabara ikitengenezwa

hapa barabara ikitengenezwa

gari zikipita pembeni kupisha ujenzi wa barabara

gari zikipita pembeni kupisha ujenzi wa barabara

Share

WANACHI WA TANDALE NA MAONI YA KATIBA

Wanachi wa tandale wengi wametoa maoni juu ya lasimu ya kwanza ya katiba na kusema muundo wa selekali tatu wao hawaiyungi mkono bora ubaki muundo uleule wa selekali mbili, pia wameunga mkono swala la mgombea binafsi pamoja na uraia wa nchi mbil, hayo yamezungumzwa kwenye kikao cha wanachama wa ccm wakijadili lasimu ya katiba, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa ccm mtogole.

mtoa mada akiwasilisha maoni kwa wanachama wa ccm

mtoa mada akiwasilisha maoni kwa wanachama wa ccm

Share

OSTAZI YASSIN AWASIHI WAISLAM WA TANDALE JUU YA MWEZI HUU MTUKUFU

Ostazi na imamu wa msikiti wa masjid bushiri amewasihi waislam juu ya mwezi huu mtukufu  na kuwambia wafanye mambo yaliyo mema na kuacha yale yote yaliyo mabaya kwani mwezi huu ni mwezi wa kuchuma, aliyasema hayo katika mauridi ya kumsifu mtume iliyofanyika tandale muhalitani.

ustazi akitoa somo juu ya mwezi mtukufu.

ustazi akitoa somo juu ya mwezi mtukufu.

waumini wa kiume wakimsikiliza ustazi

waumini wa kiume wakimsikiliza ustazi

waumuni wa kike wakimsikiliza ustazi.

waumuni wa kike wakimsikiliza ustazi.

Share