MASHINDANO YA CHIEF CUP BADO KIPIMA JOTO

Mashindano ya mpira wa miguu ya chief cup bado ni kipima joto kwa timu zinazoshiliki.timu nyingine tayali zimejiakikishia kuingia kwenye atua ya robo fainali, huku nyingine zikingojea na kuomba dua mwenzake afungwe ili yeye apite.Ukweli mashindano hayo yamekuja na sura ya tofauti kabisa na kujizolea mashabiki wengi nyakati za jioni wakishuhudia mashindano na vipaji vya vijana chipikizi.

hapa watu wamefulika uwanjani wakitizama mpira.

hapa watu wamefulika uwanjani wakitizama mpira.

hapa napo watu wapo makini kufuatilia mchezo.

hapa napo watu wapo makini kufuatilia mchezo.

Share

KUNDI JIPYA LA SANAA LAANZISHWA MTOGOLE

Kundi jipya la sanaa la KAPATE ARTS GROUP limeanzishwa, kundi hilo limeanzishwa chini ya mkurugenzi wao mwarutambi. kundi hilo linajihusisha na sanaa ya maigizo pamoja na nyimo, hivi sasa wapo katika mazoezi makali wakijiandaa kwa kushuti move yao.bado wanaitaji wasanii wa kujiunga na mazoezi wanafanya tanesco mwisho.

wasanii wakiwa kwenye picha ya pamoja

wasanii wakiwa kwenye picha ya pamoja

Share

NI WAJIBU WETU KUTUNZA MAZINGIRA

Kitendo cha kutunza mazingira ni wajibu wetu sisi wenyewe, lakini imekua tofauti kabisa watu wameanza kutupa takataka katika barabara ya kiboko bar ambayo ujenzi wake bado haujaisha, hivyo nawaomba wakazi wenzangu wa tandale sisi ndio tuwe walinzi hasa kwenye barabara yetu hiyo ambyo ilikaa muda mlefu bila kutengenezwa na tulikua hatuna ndoto kama itajengwa. Hivyo imejengwa na inapitika tuilinde ili itusaidie wote, chukua hatua  ukimuona mtu anatupa taka barabarani au akifanya kitendo chochote kile cha ualibifu.

hii ndio kiboko bar ya zamani.

hii ndio kiboko bar ya zamani.

hii ndio kiboko bar mpya
hii ndio kiboko bar mpya

 

Share

MTAA WA UZURI WAKWAMISHA ZOEZI LA MAJI YETU

Mtaa wa uzuri umekwamissha zoezi la mradi wa maji kwenda kwa wakati, wakazi hao wa mtaa wa uzuri wachache wamefukia mtaro wa kuzika mabomba kwa kigezo cha kudai kule si kata ya tandale bali ni kata ya manzese.mzozo huo uliingiliwa kati na diwani wa manzese na kufika eneo la tukio bila kutoa jibu sahihi kama kiongizi. wasimamizi wa mradi huo nao wamefika na kueleza sababu ya kuchimba hadi kule na wananchi wamewaelewa lakini hadi sasa mabomba bado hayajafukiwa chini.Mtaa wa uzuri umepakana na mtaa wa muhalitani..

huu ndio mtaro ambao umezua utata na bado kufukiwa.

huu ndio mtaro ambao umezua utata na bado kufukiwa.

mipira ya maji ikiwa nje

mipira ya maji ikiwa nje

Share

MASHINDANO YA CHIEF CUP SASA NI KUFA NA KUPONA

Mashindano ya chief cup sasa yamefikia hatua ya kufa au kupona, kwani kila timu inataka kuingia kwenye hatua ya kumi na sita (16)bora. Hivyo kila timu inapigana kiume ili kuakikisha wanashida michezo yao yote, huku timu zingine zikipoteza matumaini ya kuingia kwenye hatua ya mtoano kwa kufungwa michezo yao yote waliocheza. Mashindano hayo yameleta hamasa na changamoto kubwa hasa kwa wakazi wa tandale wakazi wa tandale wametoa pongezi kwa kamati ya mashindano na mwanzilishi wa mashindano hayo.

hapa ni mpambano ukiendelea huku mashabiki wakiangalia

hapa ni mpambano ukiendelea huku mashabiki wakiangalia

huu ndio uwanja wa mashindano mashabiki wakifuatalia mpambano

huu ndio uwanja wa mashindano mashabiki wakifuatalia mpambano

Share

VIJANA NA MCHEZO WA KAMALI

Vijana wengi wanahalibika hasa kwa kupenda michezo hatalishi kwao au kuiga vitu ambavyo si vizuri, baadhi ya vijana wengi upenda kuvuta bangi kulewa pombe na wengine kucheza kamali.

vijana wakicheza kamali na wengine wamesimama wakiwatizama wenzao.

vijana wakicheza kamali na wengine wamesimama wakiwatizama wenzao.

vijana hawa wamekutwa wamejivicha pembeni mwa mfeleji wa kiboko bar wakicheza kamali na wengine wakiwatizama wenzao, wengi wao ni wanafunzi ubana bona na pesa wanazopewa na wazazi wao uchezea kamali.IMG_5658

Share

KAMATI YA MASHINDANO YA CHIEF CUP YASTAHILI PONGEZI

baadhi ya wajumbe wa kamati ya mashindano ya chief cup

baadhi ya wajumbe wa kamati ya mashindano ya chief cup

Kamati ya mashindano ya chief cup yanayoendelea katika uwanja wa tandale elimu inastahili pongezi kubwa, hasa kwa kusimamia na kulatibu vizuri mashindano hayo bila kupata lawama yeyote ile.kamati hiyo ikiongozwa na YAHYA TOSTAU pamoja na VISENT BANABASI hadi sasa inafanya kazi vizuri kwa kufuata sheria na taratibu zote walizoweka.

Share