BARABARA YA KWA TUMBO SASA YAPITIKA VIZURI

Barabara ya kwa tumbo iyelekeayo soko la tandale sasa inapitika vizuli baada ya kuchongwa na kumwagwa vifusi, hapo zamani barabara hiyo ilikua ikinyesha mvua kidogo huwa kero kwa madeleva na wenda kwa miguu hivi sasa inapitika vizuri bila kero yeyote na nafasi kubwa kwa wenda kwa miguu.

barabara ya sokoni kabla matengezo

barabara ya sokoni kabla matengezo

Share

MASHINDANO YA CHIEF CUP YAKALIBIA KUANZA

Mashindano ya mpira wa miguu yanakalibia kuanza, kamati ya mashindo hayo ipo kwenye atua za mwisho za uhakiki wa timu na mambo mengine,mashindano yamezaminiwa na mwenyekiti wa selekali ya mtaa wa tumbo ndugu.ABDULY AZIZI a.k.a CHIEF. mashindano hayo yatafanyika katika uwanja wa shule ya msingi tandale elimu au tandale maguniani.

mwenyekiti wa mtaa wa tumbo mwenye suti ndie aliyeandaa mashindao hayo hapa yupo na viongozi wenzie.

mwenyekiti wa mtaa wa tumbo mwenye suti ndie aliyeandaa mashindao hayo hapa yupo na viongozi wenzie.

Share

KIKAO CHA MAENDELEO CHA INTERGRITY WATCH CHAFANYIKA

Wana kamati wa INTERGRITY WACH jana walikaa kikao pamoja na wenyeviti wa selekali za mitaa yote sita ya tandale, katika kikao hicho walikua wakijadili jinsi ya upatikanaji wa eneo la ujenzi wa shule katika kata ya tandale, kikao hicho kilimalizika na kupata jibu la kutafuta wadau ili wanunue maeneo kwa ajili ya ujenzi huo.kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa manyara pank wa ccm tandale.

wenyeviti wa mitaa ya tandale wakiwa kwenye kikao

wenyeviti wa mitaa ya tandale wakiwa kwenye kikao

wajumbe wa kikao wakiwa kwenye kikao.

wajumbe wa kikao wakiwa kwenye kikao.

 

Share

Nguzo za umeme za anguka Tandale

Ijumaa ya tarehe 12/ 04/ 2013 nguzo za umeme zilianguka kutokana na mvua kubwa kunyesha iliyoambatana na upepo makali. Maeneo hayo ni maeneo ya Tandale – Mharitani kuanzia Tanesco mpaka Karifonia. Ila tunashukuru Tanesco wamekuja kurekebisha.

Nguzo ambazo zimeanguka zikiwa katikati ya barabara

Nguzo ambazo zimeanguka zikiwa katikati ya barabara

Nguzo ambazo lianza kuanguka na kusababisha zingine pia kuanguka

Nguzo ambazo lianza kuanguka na kusababisha zingine pia kuanguka

 

Share

Vifusi katika barabara ya Sokoni vimesambazwa

Hapo nyuma tulitoa ripoti kuwa kuna vifusi vilivyozi barabara ya sokoni na kwa kuwa kulikuwa na mvua zikinyesha basi vikawa vibasababisha kuwe na matope mengi, na vilikuwa hapo kwa mda mrefu. Ila jana tarehe 04-04-2013 vifusi hivyo vya mchanga vimesambazwa na barabara inapitika bila matatizo. Tunashukuru sana kwa watengeneza barabara.

Share

Uchaguzi wa Kamati ya Katiba

Tandale ni miongoni mwa Kata ambazo Jana tarehe 04-04-2013 uchaguzi wa kamati ya katiba ulifanyika. Uchaguzi huo ulifanyika katika kila mtaa, hivyo kwa Tandale ulifanyika kwa mitaa minne, na kila mtaa ulichagua makundi manne yaani Vijana 2, Wanawake 2, Wazee 2 na Watu mbalimbali 2 hivyo kwa kila mtaa 1 wa tandale ulitoa watu 8. Kwa mitaa 6 Kata ya Tandale inakuwa imetoa watu 48. Tunashkuru sana kwamba Tandale tunawakilishwa na watu wengi katika Katiba.

Share