KATIBU MWENEZI WA CCM MUHALITANI APANDISHA BENDERA KWA WAJUMBE

Katibu mwenezi wa ccm tawi la muhalitani amepandisha bendera kwa wajumbe wa mashina. zoezi hilo limefanyika leo 27/01/2013 wakiwepo wajumbe 27 waliopo katika tawi hilo. Mwenezi aliambatana na kamati yake ya uenezi pamoja na vijana wa hamasa wa tawi ili kuleta shamrashamra kwa wajumbe.IMG_3996

Share

Mto ng’ombe sasa watoa samaki

Hapo kabla kipindi ambacho mto ng’ombe ulikuwa mchafu kabisa na ulikuwa unatoa harufu ilikuwa haiwezi kuleta samaki. Ila kwa sasa Mto ng’ombe ambao ulikuwa mchafu na unapitisha takataka kwa sasa unatoa samaki kwa ajiri ya kutumia nyumbani. Hii inetokana na baada ya kuysafisha na kufanya maji yanayopita ndani yawe masafi hata kuleta samaki kwa ajiri ya kupika.
image

image

Share

KUNDI LA SANAA LA WANGE UYEE ARTS GROUP LAANZA MAZOEZI

Kundi la sanaa la wange uyee arts group lenye masikani yake tandale MUHALITANI limeanza mazoezi lasmi. kundi hilo limeanza  mazoezi ya kwa ajili ya kazi zao za mbeleni. kundi hilo linatalajia kufanya muvi yao baada ya wasanii kumeza vizuri vipande vya mchezo huo. kiongozi wa kundi hilo steven paul kallage amesema bado wanaitaji wasanii wa lika zote kwa yeyote anayeitaji afike ofisini au wapige simu no.0764212212 atapewa utalatibu mzima pia amesema bado wanatafuta wazamini au wafadhili na washika dau ili waweze kuwasaidia na kuwasapoti kwa kazi zao wanazofanya.IMG_2400IMG_2397

Share

MMOMONYOKO WA MAADILI KWA VIJANA

Mmomonyo wa maadili kwa vijana wengi umekua tatizo huku tandale. vijana wengi wamekua na tabia za kuiga wazungu. watoto wakiume utawakuta wamevaa nguo inashuka hadi chini ya matako huku watoto wakike wanavaa nguo zinazoonyesha maungo yao yote. wazazi na walezi wamesema sana hadi wamechoka wakibaki wakiwatizama vijana hao wakipotea. matokeo yake vijana hao uangukia kwenye wizi kwa watoto wa kiume na wanawake kuwa makahaba. jitahada za maksudi zinahitajika kuwanusuru vijana hao.IMG_2427 IMG_2428

Share

KUNYWA KUPITA KIASI NI HATARI

Baadhi ya watu upenda kunywa pombe hadi kupita kiasi ambayo ni hatari kwao. ulevi huo usababisha mtu kukosa heshima kwa jamii, watoto na familia ya kwa pamoja. muda mwingine hata ukiwa na jambo la msingi hutosikilizwa kutokana na ulevi wa kupita kiasi na unakuwa uchagui pakulala ukishalewa au kubakwa na kulawitiwa na wauni. pombe ukufanya kuwa mzee ata ukiwa kijana.IMG_3959 IMG_2323

Share

AKILI NI NYWELE KILA MTU ANA ZAKE

Kijana huyu amekutwa akinawa maji ya mvua iliyonyesha na kutwama huku watu wakimtizama hiyo ni hatari kwake. IMG_2466haikuweza kufamika vizuri kama ni chizi au ana akili timamu. hiyo mala nyingi inatokea kwa watoto inaponyesha mvua wao uogelea huku wakishangilia huku wazazi wakiwatizama na wapita njia wakiwashangaa. au muda mwingine kutokana na shida ya maji watoto hao utumwa na wazazi wao wachote maji yanayotililika kutoka kwenye mabati.

Share

WANAFUNZI WAFUNGUA SHULE NA KUANZA MASOMO

Wanafunzi wamefungua shule na kuanza masomo. mara nyingi kipindi cha kufungua shule kunakuwaga na maudhulio machache kwa wanafunzi kutokana na wengine kuwa bado mikoani au malalamiko ya wazazi kutokuandishwa watoto wao wanaoanza darasa la kwanza kwa kigezo nafasi kujaa. katika hayo hakuna hata moja lililojitokeza kwenye shule za tandale ambazo ni tandale elimu, tandale hekima, tandale magharibi na tandale muhalitani.IMG_2516IMG_2515

Share

WAGENI NA MAENDELEO YA TANDALE

Wageni wa kutoka nchi za nje mara nyingi upenda kuja kutembelea tandale na kuangalia changamoto zinazowakabili wana tandale. Wanaguswa sana pale wanapotembezwa katika mitaa na kuangalia maendeleo yao wakazi wa mitaa hiyo. Baada ya ziara zao uahidi kurudi na kuleta miradi ya kusaidia tandale wakipata Pesa za miradi.

Mark (kulia), Gary (katikati) na Ashiru (kushoto) wakitembelea maeneo ya Tandale Sokoni.

Mark (kulia), Gary (katikati) na Ashiru (kushoto) wakitembelea maeneo ya Tandale Sokoni.

Mark akijaribu kupepeta Mahindi katika kiwanda kimoja kilichopo maeneo ya Tandale Sokoni

Mark akijaribu kupepeta Mahindi katika kiwanda kimoja kilichopo maeneo ya Tandale Sokoni

Share

HATARI YA MAGONJWA YA MLIPUKO TANDALE

Kipindi hiki cha mmvua zinazoendelea kunyesha kuna hatari ya kutokea magonjwa ya mlipuko katika kata ya tandale. mara nyingi mmvua zinaponyesha baadhi ya watu ufungulia mitaro yao na kusababisha maji kusambaa ovyo na wengine kutupa taka katika mitaro na mitaro hiyo kuziba na maji kutililika katika makazi ya watu.hali hiyo ni hatali zaidi kwa watoto ambao wao mmvua ikinyesha upenda kuogelea.IMG_3751IMG_3057 IMG_2471

Share