TAMASHA LA UKIMWI LAFANYIKA TANDALE

Tamasha la ukimwi limefanyika katika kata ya tandale mpakani na manzese. tamasha hilo lilikuwa la aina yake lililofanyika katika uwanja wa fisi, watu wengi walijitokeza na kupima kwa hiari na kufualhia huduma hiyo. tamasha hilo ni mfurulizo ya matamasha ya kuendea siku ya ukimwi dunia inayofanyika 1/12/2012 watu walijionea burudani mbalimbali zikiwemo za ngoma na maigizo zilizotolewa na kundi la wange uyee arts group la tandale muhalitani pamoja na show za watoto na wakubwa.

Share

WANA TANDALE LEO WAMETOA MAONI YAO JUU YA KATIBA MPYA

Wana tandale leo wametoa maoni yao juu ya katiba mpya. kila mmoja alitoa mchango wake na maoni yake bila kuzomewa au kuchekwa ila zaidi mtu akiongea hoja ya msingi wanampigia makofi hicho ndicho kilichofanyika tandale leo na wengine walishiliki kwa kujaza fomu na kutoa maoni  yao . hata ilipofika mwisho msimamizi alitoa sukrani za pekee kwa wana tandale kwa kutoa maoni mazuri juu ya katiba mpya na kuwasisitiza wasome vipeperushi walivyopewa kwani mchakato bado unaendelea.

Share

Sanitation Hackathon Dar es Salaam yatembelea Tandale

Leo Tandale imetembelewa na wageni kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo Benki ya Dunia  pamoja na mashirika mengine. Ugeni huu umehusisha wataaram wa aina tatu nao ni:- Watu wa GIS (Geographical Information System), watu wa Information Technology (IT) pamoja na watu wa Journalism. Thumuni kubwa la ugeni huo lilikuwa ni kujua hali halisi ya vyoo katika eneo la Tandale na kujua njia wanazozitumia viongozi wa tandale ili kupata taarifa kutoka kwa wananchi wao ili kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayotokea. Ugeni huo ulitembea ofisi ya Mtaa wa Mkunduge na kuelezewa hali halisi ilivyo mtaani hapo ambapo baadae walitembelea eneo hilo ili kujionea hali halisi ya vyoo. Ugeni huo ni kukamilisha maandalizi ya mashindano yanayotegemewa kufanyika nchi nyingi ikiwemo Tanzania lengo likiwa kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanatokana na vyoo.

Share

WATOTO NA MAISHA

Watoto wengi ukosa malezi bora na elimu kutokana na ugumu wa maisha ujikuta uingia katika kujitafutia maisha aiza kutumwa na wazazi wao au wao wenyewe. watoto hao wengi wao uokota chupa za maji au vyuma chakavu kwenda kuuza wengine utafuta pesa ya shule na wengine ukatisha masomo na muda mwingine ukosa laha huwa wapweke na uwa na mawazo mengi wakipumzika.

Share

WANA TANDALE TUJITOKEZE KWA WINGI 26/11/2012 KUTOA MAONI YA KATIBA MPYA

Wana tandale tunatakiwa tujitokeze kwa wingi siku ya 26/11/2012 kwenye viwanja vya shule ya msingi tandale elimu ili kwenda kutoa maoni yetu juu ya katiba mpya. hii ni nafasi pekee kwetu kwani mawazo yako ni muhim sana ukipata taalifa hii mjulishe na mwenzio muda ni saa 8 mchana hadi saa 11 jioni usikose kufika.

Share

KINA MAMA NA UJASILIA MALI

Kina mama na ujasilia mali imekuwa changamoto moto kwao ya kujikwamua na maisha kina mama wa mtaa wa kwa tumbo wamekutwa wakitengeneza sabuni ya ya maji dawa ya choo pamoja na shampoo ili wakauze wajipatie kipato. kina mama hao wamesema wateja zao wakubwa ni kina mama wenzao pamoja na baadhi ya makampuni ya usafi hivyo inawaomba watu wajitokeze ili kuwatafutia masoko makubwa pia vile vile wanatoa ilimu na mafunzo ya utengenezaji wa vitu hivyo.

Share

KUNDI LA SANAA LA WANGE UYEE LAJIPANGA UPYA

Kundi la sanaa la wange uyee arts group lenye masikani yake mtaa wa muhalitani linajipanga upya baada kazi zao kufeli sokoni. kundi hilo lenye fani ya uigizaji ngoma za asili  sarakasi pamoja na nyimbo. wanajipanga kucheza film nyingine pia inawaomba wadau na wafadhili na wapenzi wapenda sanaa wajitokeze ili kulizamini kundi hilo liweze kufikia malengo.

Share