USAFI WA MIFELEJI

Halimashauri ya manispaa imeanza usafi wa mifeleji na mitaro iliyo barabarani ambayo ilikuwa kero kubwa sana mifereji hiyo ilikuamichafu sana hadi kufikia wakazi wanaokaa na mifereji hiyo kuchangishana pesa na kuwapa vijana ili waisafishezoezi hilo limefanyika katika mitaa ile ambayo ipo karibu na barabarakatika kata ya tandale.

Share

MWIZI APIGWA MUHALITANI

Mwizi amepigwa na watu wenye hasira kari, tukio hiro limetokea majira ya saa kumi na moja usiku mwizi huyo inasemekana walikuwa wawili yeye na mwenzie walimkaba mtu na kumuibia pesa laki mbili na simu ya mkononihivyo baada ya kupatikana alipelekwa hadi kwenye ofisi ya selekali ya mtaa na kuanza kumpiga hadi polisi walipokujana kumchukua na kuondoka nae.

Share

UPANUZI WA MTO NGOMBE

Katika mitaa ya muhalitani mtogole na mkunduge umeanza uanuzi wa mto wa ngombe,mto huo zamani ulikuwa mkubwa na ulikuwa ukipitisha maji vizuri hata kipindi cha mafuliko maji yalikuwa hayasambai hovyo, lakini baada ya watu kujenga nyumba na kutupa taka karibu na mferejina kumechangia mto huo kuwa mdogo hata mafuliko yanapokuja maji husambaa, wanachi wa maeneo hayo wamefulahishwa na kitendo cha upanuzi wa mto huo na kutoa ushilikiano kwa viongozi wa mitaa yao.

Share

AJIRA BADO TATIZO SUGU

Japokuwa vijana wengi wameamua kujiajiri wenyewe katika kazi tofauti kwa kuangalia fursa zilizopo katika maeneo yanayowazunguka. kama vile kuendesha baiskeli za mizigo za magurudumu matatu, Pikipiki za matairi mawili maarufu kama bodaboda na za matairi matatu maarufu kama bajaji kwa kubeba abiri, na wengine kusukuma vitoroli vya mizigo lakini hali bado ngumu kwa upande wao

hali hii imeonekana katika maeneo ya soko la Tandale ambapo vijana hao walikutwa wamekaa tu na vyombo vyao vya usafiri bila ya wateja. wengi wao walikuwa na simanzi na hawakujua nini suluhisho la tatizo hili.

 sisi hatuchagui kazi bwana. na wala hatusubiri kuajiliwa. Tunajua huku kwetu Tandale hakuna viwanda wala makampuni. eneo letu kubwa la kujidai ni soko lakini napo ni pagumu kama unavyoona tumekaa tu hatujapata kazi toka asubuhi.

walisema baadhi yao

hii ni hali halisi ya hapa kwetu

 By Salum Kaponda From Tandale Community

Share

Madaraja ya Tandale

Kata ya Tandale ni eneo ambalo maeneo yake mengi yako bondeni hivyo husababisha kuwe na maji mengi kipindi cha mvua hasa maeneo ya bondeni (mitaroni) ambapo maji yanajaa sana kipindi hicho. Ukiangalia madaraja mengi yaliyoko Tandale hayakidhi maji yanayopita hasa wakati wa Mvua (maji mengi) hivyo husababisha watu kupata shida kupita kipindi cha mvua kwa kuwa madaraja mengi yakuwa yanapelekwa na maji.

By Msilikale

Share

Si sawa wanavofanya waendesha bodaboda

Katika barabara ya morogoro ambayo kuna utengenezajia wa barabara kubwa nimekuta waendesha bodaboda wamepanga mawe na wakichangisha hela (Shiling 100) ili kuruhusu wanachi kuvuka sehemu ambayo ina maji baada ya mvua kunyesha Dar es salaam. Hali hii sio nzuri maana sidhani kama wananchi wanatakiwa kulipa hela ili kuvuka sehemu ambayo ni barabara. Kama ndo ivo basi inabidi wanaotengeza barabara haraka ili watu waweze kupita barabarani bila hela.

 

Share