SHIDA YA MAJI KATIKA MTAA WA MTOGOLE.

Mtogole ni moja ya mtaa kati ya mitaa sita inayopatikana katika kata ya Tandale,ni mtaa ambao unamatatizo mengi sana lakini hili la maji limekuwa zaidi.Ni kweli kabisa kwamba nchi nzima ina tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama lakini kwa upande wa mkoa wa Dar es salaam hasa katika mtaa wa Mtogole iliyo katika kata ya Tandale wilaya ya Kinondoni inaonekana kuwa ni zaidi.

Wakazi wa mtaa huu mara nyingi wameonekana wakihangaika kutafuta maji na mara nyingine inawalazimu kutembea umbali mrefu (nje mtaa wao) kwa ajili ya kutafuta maji,pamoja huwa wanayapata lakini kiwango wanachokipata hakilingani na mahitaji yao kwa sababu kuu mbili,ya kwanza ni kuwa kutembea umbali mrefu kunawafanya wachoke kwa haraka hivyo kutokuwa na nguvu ya kutosha kuchota maji mengi, na sababu ya pili kuwa hayo maji pia huwa hayauzwi kwa bei ambayo wameizoea(ndoo ya lita 20 kwa Tsh 100/=) lakini ukubwa huohuo wa ndoo huuzwa kwaTsh 500/=.

Kipato cha mtanzania wa kawaida kwa siku ni chini ya dola moja,na kwa sasa dola moja ni sawa na Tsh 1600/= hivyo tunaona kuwa mtanzania huyu kwa siku kipato chake ni chini ya Tsh 1600/=, lakini mtanzania huyu hapatikani sehemu nyingine isipokuwa kwa Mtogole!Je, kama kwa siku anapata Tsh 1600/= au chini ya hapo ni kiasi gani cha pesa atakitenga kwa ajili ya maji,chakula,pango na nk?

Yote tisa,kumi ni sehemu ambazo maji hayo yanapatikana,mipira inayopitisha maji hayo imepita sambamba na mifereji ya maji taka na wanaojiita wamiliki wa mipira hiyo huwa wanaikata na kuuza maji katika mifereji hiyohiyo ya maji taka, na kuna baadhi ya matangi ya maji(water pointi) yapo karibu na vyoo,je homa za matumbo na kuharisha zitakwisha mtaani kwetu?

Je,ni upi wajibu wa mwananchi wa Mtogole ikiwa ni haki yake kupata maji safi na salama?

Je ni upi wajibu na nini ni haki ya serikali kwa wananchi wa eneo hili!

By

Chillu

Share

 Imeandaliwa na kuandikwa na;

Chillumanga!

Share