Mazalia ya mbu

Maeneo mengi Tandale yamezungukwa na mifereji ya maji taka, mifereji hiyo maji hayatembei kutokana na wananchi kutupa taka kwenye mifereji hivyo husababisha maji kutuama na mbu kuzaliana. Hali hii inaweza kusababisha magonjwa kama maralia, kichocho na magonjwa mengine.

 


Share

watoto wacheza maeneo hatalishi

leo tumewakuta watoto wakicheza maeneo hatalishi, watoto hao tumewakuta maeneo ya kiboko bar mtaa wa mtogole, Maeneo hayo mala nyingi huwa kuna nyoka ambao wanaweza kumzuru mtoto wakati wowote, Pia kuna mifereji ya maji taka yanayotililika kutoka vyooni ambayo yanaweza kusababisha magonjwa hatalishi kama, kaharisha, kichocho, kipindupindu na magonjwa mengine ya mlipuko.

Share

Mashindano ya kusoma Qur-an kata ya Tandale

Leo, kulikuwa na mashindano ya kusoma Qur-an ambayo yamefanyika Tandale katika mtaa wa Sokoni yakihusisha watoto wa miaka saba hadi kumi na tano. Mashindano haya mara nyingi hufanyika kipindi cha mwezi wa ramadhani, ambayo yameandaliwa na jumuiya ya vijana wa Kiislam Tandale. Hii ni kuwezesha watoto na vijana kuhifadhi maneno ya Kiislam na kuwezesha kuwa na imani ya kiislam wakiwa bado wadogo. Katika mashino hayo washindi wanategemewa kupewa zawadi kutoka kwa mgeni rasmi ambae ni Diwani wa kata ya Tandale. Mshindi wa kwanza anategemewa kupata Baiskeri, Msaafu, Juzu 3 na 35,000/-, mshindi wa pili anategemewa kupewa Baiskeri na Musahafu, na mshindi wa tatu anategemewa kupewa Pasi ya umeme, musaafu na saa ya ukutani.

Share