ULINZI SHILIKISHI WAPUNGUZA WIZI TANDALE

Ulinzi shilikishi ulioanzishwa na viongozi wa selekeli za mitaa katika kata ya tandale umesaidia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa wizi wa uporaji uliokuwa umeshamili kwa kiasi kikubwa hasa nyakati za asubuhi.
Vijana hao wa ulinzi wameonekana wakifanya kazi zao vizuri na kuwakamata baadhi ya wezi wanaotaka kuiba,hivyo wa kazi wa tandale kwa sasa wako huru wanaposhuka kwenye magari na asubuhi wanapokwenda kupanda magari kwani ndio muda walio kuwa wakiporwa zaidi
Viongozi wa mitaa wanawaomba wananchi kutoa kuishilikiano kubaini waalifu na kutoa michango ya ulinzi ili zoezi hilo liwezi kudumu zaidi.

gari la polisi likimchukua mtuhumiwa aliyekamatwa na vijana wa ulinzi shilikishi tandale.

Share

DARAJA LAVUNJIKA TANDALE

hili ndio daraja la kwakarama lilirovunjika kwa kupinda.


Daraja linarounganisha kati ya tandale na kijitonyama,lilipo katika mtaa wa muhalitani eneo la kwakarama jana limekatika kutokana na vua kubwa kunyesha na kusababisha maji kujaa hadi juu ya daraja na kusababisha daraja hiro kuvunjika.
daraja hiro ni njia kubwa sana kwa waenda kwa miguu na ndio nyepesi kufika kijitonyama kwa haraka, hivyo kuvunyika kwake kumeleta hatha kubwa kwa wananchi,pamoja na kuvunjika kwa daraja hiro watu wengine walikuwa wakifosi kupita hivyo hivyo jambo ambaro ni hatali sana kwa usalama wao.
pamoja na daraja kuvunjika daraja lakini baadhi ya nyumba nazo zilivamiwa na maji na kusababisha watu kuhamisha vitu vyao na kuhama wao kwa muda.

Share

MWENYEKITI CCM WILAYA YA KINONDONI AFANYA USAFI

Mwenyekiti wa ccm wa wilaya ya kinondoni mhe, Salumu Madenge jana 4/2/2017.ameshilikiana na wakazi wa tandale katika kufanya usafi, usafi huo umefanyika katika hospital ya tandale.
zoezi hilo limefanyika huku wapenzi na wanachama wa ccm wakiwa wamevaa sale kwa ajili kuazimisha miaka 40.ya kuzaliwa ccm.
baada ya kumalizika zoezi hilo mwenyekiti aliwahutubia wanachama wate wa ccm na kutoa historia fupi ya chama kilipotoka na mazuri mengi yaliyofanywa na chama.

Huyu ni mwenyekiti wa ccm kata ya tandale mhe,Tamim omari na Ashiru issa

Share

TAWI LA RED CROSS TANDALE LAZINDULIWA

Kikundi cha Tandale red cross zuia mafuliko leo 28/1/2017 kimmezinduliwa lasmi na kuwa tawi kamili la red cross, uzinduzi huo umefanyika katika ofisi ya afisa mtendaji kata ya tandale na kushuhudiwa na viongozi wa selekali ya mtaa na watendaji wa mitaa na pia katika uzunduzi huo wanachama walifuahi sana baada ya kuuona uongozi wa red cross ulipowasili.
Baada ya kufika uongozi wa red cross walikalibishwa na wenyeji wao na kuzindua tawi na kuwakabithi bendera katiba na kadi za uanachama ppamoja na kutoa vyeti kwa wanachama, tawi hiro kwa sasa lina wanachama 30 halijafunga milango linawaruhusu watu wengine kuja kujiunga.

Share

NYUMBA YAUNGUA

Tukio hiro la kuwaka moto nyumba limetokea 14/01/2017 katika mtaa wa muhalitani kata ya tandale mida ya saa moja asubuhi, baadhi ya mashuhuda waliokuwepo katika tukio hilo wamesema chanzo cha moto huo ni kipande cha moto uliokuwa haujazimwa.
baada ya kuona moto wanachi walijitokeza kwa wingi ili kuuzima moto huo, walifanikiwa kuuzima moto huo huku vyumba viwili vikiwa tayali vimeshaungua.IMG_0013

Share

MCHACHUKO PRODUCTION WAFANYA MOVIE

Kikundi cha Mchachuko jana 5/12/2016 wameingia mtaani kushuti movie yao inayojulikana kwa jina la Choo cha Ulithi katika movie hiyo wamewashilikisha wasanii wakongwe wa Comedy kama Ringo, Tin weat Mzee sumaku Kidi na Zimwi.
Viongozi wote wa kundi hilo mr Mkwayu na Meshack wamesema movie hiyo iko vizuri wale wapenzi wakae mkao wa kula kwani baada ya kukamilika kushuti itakwenda editing kisha itaingia sokoni.
Wanawaomba watanzania itapoingia sokoni wawaunge mkono kwa kununua ili kwani wakifanya hivyo ndio itakuwa vizuri kwao kwa kufanya kazi nyingine.

Hapa wasanii wakiwa kwenye scene wakiigiza

Hapa wasanii wakiwa kwenye scene wakiigiza

Hapa wasanii wakiwa kwenye scene wakiigiza

Hapa wasanii wakiwa kwenye scene wakiigiza

Share

MAJI YAZAGAA MTAANI TANDALE

Maji safi na salaama ya Dawasco yame kuwa kero kubwa kutokana na kuzagaa mitaani na kuababisha magari na watu kupita kwa tabu baadhi ya sehemu,tatizo hilo linakuja kutokana na mabomba kuchakaa na kuvujisha maji.
viongozi wa mitaa ujitaidi kutoa taalifa kwa watu husika na wakija wanashuhulikia tatizo na baada ya siku chache tatizo uanza tena na kuleta kero tena.
tunawaomba wanahusika kulitizama tatizo hili kwa mapama kwani maji ni muhim sana hivyo tunavyoona yanamwagika huku wengine wakiyatafuta kwa galama kubwa.
maeneo yanayomwagika maji ni muhalitani, sokoni na mtogole naamini viongozi husika watalifanyia kazi tena kwa wakati ili kuondoa usumbufu kwa wananchi.

hili ni shimo la maji limechimbwa kwa ajili ya kuyafunga maji yanayozagaa.

hili ni shimo la maji limechimbwa kwa ajili ya kuyafunga maji yanayozagaa.

Share

WATOTO NA USALAMA WAO

Watoto wengi wanapenda kucheza ili kujifulahisha katika michezo hiyo ipo mizuri na mibaya na nihatali kwao, kwao hiyo wanaitaji ulinzi na uangalizi wanapokuwa katika michezo yao.
Katika mto ngombe watoto hupenda sana kucheza lakini sio sehemu salama kwao kwani sehemu hiyo kuna wadudu wabaya na chupa zilizovuchika zinaweza zikawakata.
Wito kwa wazazi na walezi tuwachunge watoto wanapokuwa kwenye michezo yao ili kuwaepusha na majanga.

hapa watoto wakicheza juu ya mti.

hapa watoto wakicheza juu ya mti.

Share